Ukiwa hapa kwetu, ukivaa hivyo vitu utaonekana umeenda kinyume na matakwa ya imani. Lakini ukiwa nchi za magharibi, hakuna mtu atakayeshangaa ukivaa vitu hivyo maeneo ya ibada!
Hayo mavazi uliyoongelea sio asili yetu, asili yetu ni nguo za kupima kwa fundi (wengine wanasema special), na tulizoeshwa hivyo tangu ukoloni. Na hata Mwalimu nyerere alipochukua nchi toka kwa wakoloni, alituelekeza tuwe na mapenzi ya kipenda vya kwetu.
Unaweza kukumbuka viwanda kama Mwatex, Mutex, Urafiki, nk. Viwanda hivi vyote vilikuwa vya kutengeneza nguo kwa ajili ya Watanzania, na wengi wetu tulizoea nguo hizi. Nakumbuka wakati nasoma shule moja jijini Tanga (kipindi hicho halikuwa jiji), tulikuwa tunavaa kaptula za khaki. Nguo hizi zilikuwa zinatoka katika viwanda hivi.
Akina mama wengi, walikuwa wanavaa vitenge na khanga zilizotengenezwa na viwanda hivi. Na bidhaa zenyewe zilikuwa na viwango vizuri na watu (Watanzania) walizipenda sana.
Hizo nguo ulizotaja zimekuja baadae sana kama mitumba na zilikuwa chache, na hii ikafanya watu wachache kuwa nazo. Kwa hiyo, mtu akionekana na nguo hiyo mahali pa ibada walimshangaa.
Kwahivi, ni utamaduni tu na si vingine vyo. Unaweza kuvaa nguo yoyote ili mradi inasitiri maungo yako. Mungu haangalii umevaa nguo gani, bali matendo gani unafanya ili kutimiza mapenzi yake!