Ni sahihi kuwapiga picha watu wanaopewa msaada kidini?

Ni sahihi kuwapiga picha watu wanaopewa msaada kidini?

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Biblia inasema "unapotoa msaada kwa mkono wa kulia hakikisha mkono wako wakushoto haujui"

Kama nitakua nimekosea mtanisahihisha na wajuzi wa Islamic waje wadadavue Nini nini miongozo wa Qur'an tukufu kuhusu kupiga picha watu wanaopewa msaada nakusambaa mtandaoni.

Nawasilisha swali langu.

1680631851993.jpg

Kiukweli sadaka ya kutangaza au kujionyesha hiyo malipo yake hapa duniani Kwa maana utasifiwa kuwa umetoa lkn Kwa Allah haisomeki

Ila

Ninachoona kuna mazingira Fulani ambayo wafadhili wanatoa misaada sasa wanataka kuona je imewafikia walengwa?

Sasa kama hiyo ndio Nia Yao basi watapata malipo Yao inshallah lkn kama kujionyesha Kuwa wao ni watoaji basi hakuna thawabu hapo.
 
Hilo andiko la mkono usiuone mkono mwenziye lipo katika Biblia katika kitabu gani??-- naomba nukuu kwanza kabla sijachangia maoni yangu.
 
Kiukweli sadaka ya kutangaza au kujionyesha hiyo malipo yake hapa duniani Kwa maana utasifiwa kuwa umetoa lkn Kwa Allah haisomeki

Ila

Ninachoona kuna mazingira Fulani ambayo wafadhili wanatoa misaada sasa wanataka kuona je imewafikia walengwa?

Sasa kama hiyo ndio Nia Yao basi watapata malipo Yao inshallah lkn kama kujionyesha Kuwa wao ni watoaji basi hakuna thawabu hapo.

Umejibu vizuri sana chief, ila napenda niongezee kidogo hapo, kutoa kwa aina hiyo pia ni mafunzo na hamasa kwa watu wengine wenye uwezo wa kutoa nao watoe ili wapate radhi na thawabu kutoka kwa Allah, katika kutoa ni Allah pekee ndiye anayejua siri za nia za kutoa kwetu.
 
Umejibu vizuri sana chief, ila npenda niongezee kidogo hapo, kutoa kwa aina hiyo pia ni mafunzo na hamasa kwa watu wengine wenye uwezo wa kutoa nao watoe ili wapate radhi na thawabu kutoka kwa Allah, katika kutoa ni Allah pekee ndiye anayejua siri za nia za kutoa kwetu.
Swadakta chief
 
Leo tu nimetoka kushuhudia jambo kama hili, yaani hivihivi unasimamishwa na mizigo yako unapigwa picha.

Binafsi hili jambo linanikera sana, japo siwezi kuvaa viatu vya hao watoaji au hao wanaosimamia hayo mambo, maana kwao huonekana ni muhimu sana kupiga picha.

Lakini hatakama itakuwa hawafanyi hivyo kwa ria, lakini hili suala linawatia dhiki sana hao wanaosaidiwa, hebu watazame hata hao namna walivyokaa.
 
Kweli kabisa stara ni kitu muhimu Sana kwakweli.
Hata kama Mimi nikazam pm kwako unibust hlf unakuja hapa barazani unasema umenibust wallah nitakumaind
 
MATHAYO 6:2

Basi, unapomsaidia maskini, usijitangaze. Usifanye kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani ili watu wawasifu. Kweli nawaambieni, hao wamekwisha pata tuzo lao

Lakini umeshapewa jibu la jambo hilo, jibu hilo hapo 👇🏻

Kiukweli sadaka ya kutangaza au kujionyesha hiyo malipo yake hapa duniani Kwa maana utasifiwa kuwa umetoa lkn Kwa Allah haisomeki

Ila

Ninachoona kuna mazingira Fulani ambayo wafadhili wanatoa misaada sasa wanataka kuona je imewafikia walengwa?

Sasa kama hiyo ndio Nia Yao basi watapata malipo Yao inshallah lkn kama kujionyesha Kuwa wao ni watoaji basi hakuna thawabu hapo.
 
Juzi nilipita msikiti fulani nikakuta nyomi ya watu wamepanga foleni nikawa najiuliza leo kuna kiongozi gani mkubwa wa dini ametembelea huu msikiti.

Kucheki pembeni nikakuta kuna sheikh kanyuka kanzu safi afu uchebe umejaa kiasi akifumba mdomo wakikuambia kautafute hauupati

Uchebe umepakwa bleach mkono wa kushoto kashika rozali isiyokuwa na msalaba afu mkono wa kulia kabeba Canon yenye lens flani hivi kubwa mara nyingi nimekuwa nikiwaona vijana wa Millardayo wakizishika.

Wakati nimezubaa ndio nikasikia kuwa huyo sheikh anapiga picha hao waliopo kwenye foleni wanaopokea msaada.

Nilipouliza kwanini wapigwe picha wakati hii ni sio taasisi ni dini na haikupaswa kuwa na elements za kuchoreshana, jamaa alinijibu hivi.

Aliniambia wanao fund hiyo misaada ni waarabu wa nje, wao wanatoa kiasi cha pesa ambacho wanawakabidhi viongozi wa msikiti husika ila wanataka kuthibitisha msaada waliotoa umetumika kama walivyotaka. Ndio hapo wanahitaji kuona picha kama uthibitisho

Kwa hiyo wanaopanga hizo foleni hawawezi kuchoreshwa kwenye big screen za umma, bali wataonekana kwa wahusika walio fund hiyo misaada

So unao uchaguzi, ubaki na ustaarabu wako wakugoma kuanikwa kwa waarabu ukaji faitie kivyako kupata hayo mahitaji au ule buyu ujikaushe kwenye foleni afu umuache Millardayo afanye kazi yake
 
Back
Top Bottom