Ni sahihi kuwapiga picha watu wanaopewa msaada kidini?

Ni sahihi kuwapiga picha watu wanaopewa msaada kidini?

Hiyo ni hadithi ya mtukufu mtume Muhammad (saw) ndiyo inasema hivyo sasa leo nashangaa kusikia kwamba hadithi hiyo pia imo kwenye Biblia.
Mwamba kanisaidia mkuu [emoji123]

Mathayo 6:3

Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kulia
 
Hiyo ni hadithi ya mtukufu mtume Muhammad (saw) ndiyo inasema hivyo sasa leo nashangaa kusikia kwamba hadithi hiyo pia imo kwenye Biblia.
Itakua vizuri Kama na wewe ukitupa hiyo hadithi ili tuendeleee kujifunza mkuu.[emoji41]
 
Sio sahihi hakukua na haja ya kuwapiga picha wao wametaka kutoa sadaka ya ftar wangetoa bila kuwadhalilisha kuwapanga na mstari kabisa
Kupiga picha muhimu kuzuia utapeli

Wengine unakuta uwezo wanao wanafoji kupokea misaada wakati wako vizuri tuvizuri waonekane wazi wanaopewa dunia iwaone na kila atakaye uthibitisho awaone

Watoa misaada wengine matapeli hutapeli wafadhili ohh naomba misaada nipelekee yatima anafisadi yote anarudisha ripoti kwa wafadhili kuwa alitoa kumbr hakutoa

Picha muhimu tena watu wakipigwa wasifiche nyuso zao
 
Mwamba kanisaidia mkuu [emoji123]

Mathayo 6:3

Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kulia
Hiyo ni sadaka kanisani huko
 
Kiukweli sadaka ya kutangaza au kujionyesha hiyo malipo yake hapa duniani Kwa maana utasifiwa kuwa umetoa lkn Kwa Allah haisomeki

Ila

Ninachoona kuna mazingira Fulani ambayo wafadhili wanatoa misaada sasa wanataka kuona je imewafikia walengwa?

Sasa kama hiyo ndio Nia Yao basi watapata malipo Yao inshallah lkn kama kujionyesha Kuwa wao ni watoaji basi hakuna thawabu hapo.
Wanaonaje? Kwa hizo picha?
 
Kupiga mujimu kuzuia utapeli

Wengine unakuta uwezo wanao wanafoji vizuri waonekane wazi wanaopewa

Watoa misaada wengine matapeli hutapeli wafadhili ohh naomba misaada nipelekee yatima anafisadi yote anarudisha ripoti kwa wafadhili kuwa alitoa kumbr hakutoa

Picha muhimu tena watu wakipigwa wasifiche nyuso zao
Kwa nini wasipige na kupeleka moja kwa moja kwa hao ''wafadhili''? Kama una macho nadhani umeona neno ''wafadhili'' nimeliandikaje.
 
Biblia inasema "unapotoa msaada kwa mkono wa kulia hakikisha mkono wako wakushoto haujui"

Kama nitakua nimekosea mtanisahihisha na wajuzi wa Islamic waje wadadavue Nini nini miongozo wa Qur'an tukufu kuhusu kupiga picha watu wanaopewa msaada nakusambaa mtandaoni.

Nawasilisha swali langu.

Ubinadamu kazi!

Mathayo 6
1 Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni.

2 Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu.

3 Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume;

4 sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

5 Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao.

6 Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

7 Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi.

8 Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba.

9 Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,

10 Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.

11 Utupe leo riziki yetu.

12 Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.

13 Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]

14 Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.

15 Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.

16 Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao.

17 Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso;

18 ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

19 Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba;

20 bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi;

21 kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.

22 Taa ya mwili ni jicho; basi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote utakuwa na nuru.

23 Lakini jicho lako likiwa bovu, mwili wako wote utakuwa na giza. Basi ile nuru iliyomo ndani yako ikiwa giza; si giza hilo!

24 Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.

25 Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?

26 Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao?

27 Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?

28 Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti

29 nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.

30 Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?

31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?

32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.

33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.

34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.
 
Kwa nini wasipige na kupeleka moja kwa moja kwa hao ''wafadhili''? Kama una macho nadhani umeona neno ''wafadhili'' nimeliandikaje.
Vizuri hata jamii inayowazunguka iwaone ndio inawajua vizuri kama kweli wahitaji

Wanaficha nini kama wao wahitaji wapokea misaada kuna shida gani jamii ikiwaona

Tena kipindi hiki cha Ramadhani wenye.nacho wanaibiwa sana na matapeli wasio na uhitaji kwa kuchukua misaada ya vyakula,sukari ,tende nk kupeleka makwao

Kamera zitumike sana tena sio za picha tu hadi za video na zionyeshwe hadi misikitini kuonyesha waliopokea hiyo misaada eneo husika na kwenye TV na kwa wafadhili
 
Mawazo ya kiarabu haya. Siku zote utamaduni wa kiarabu umejikita sana kwenye ubwana na utwana. Hata hadithi nyingi zenye asili ya huko zinasimulia juu ya u-bwana na u-twana.
 
Wanaonaje? Kwa hizo picha?
Picha irudiwe kupigwa hao wapokea misaada walioficha nyuso zao waambiwe wanyanyue sura juu Zionekane kwenye kamera

Wao ni wahitqji wanaficha sura kwa nini?
Mhitaji kweli hafichi sura

Wapiga picha wanaotoa misaada wawaambie kabisa wanaopokea sharti sura zao zionekane wazi kwenye picha wakipokea
 
Mawazo ya kiarabu haya. Siku zote utamaduni wa kiarabu umejikita sana kwenye ubwana na utwana. Hata hadithi nyingi zenye asili ya huko zinasimulia juu ya u-bwana na u-twana.
Kukubali kusaidiwa ukiwa na shida kweli hakuna cha ubwana na utwana hapo

Ukipokea msaada ukapigwa na picha kopi akondoka nayo na wewe ukapewa yako ukabandikwe kwenu ukutani kama picha ya ukumbusho ukipokea msaada kuna shida gani

Pokea huku na picha inachukuliwa ukipokea
 
Itakua vizuri Kama na wewe ukitupa hiyo hadithi ili tuendeleee kujifunza mkuu.[emoji41]

Mkuu hiyo hadithi ni ndefu na mwishoni mwake ndio kuna hicho kipande, ili kuipata naombaa Google kwa Title hii:- "The seven persons who will be under the shade of All in the judgment day."
 
Ukitaka usidhalilike ukatae msaada kwa nguvu zote; sio msaada unataka, kupigwa picha hutaki; kama ni hivyo kataa vyote.
Kua uyaone mwanangu. Dunia uwanja wa fujo. Ukiona unashiba wewe shukuru. Nakubaliana na wewe kuwa kuombaomba siyo jambo zuri hasa kama mtu una uwezo wa kufanya kazi, ila kuna scenario nyingine mtu anafikia kwenye stage ya kuomba kwa sababu mbalimbali zisizozuilika.
 
Biblia inasema "unapotoa msaada kwa mkono wa kulia hakikisha mkono wako wakushoto haujui"

Kama nitakua nimekosea mtanisahihisha na wajuzi wa Islamic waje wadadavue Nini nini miongozo wa Qur'an tukufu kuhusu kupiga picha watu wanaopewa msaada nakusambaa mtandaoni.

Nawasilisha swali langu.

SI sahihi ila unakuta wanaotoa msaada siku hizi wanahitaji angalau ushahidi Ili wajiridhishe mana upigaji mwingi.
Mfano misikiti ikiwa inajengwa Kwa misaada hua warabu wanataka kupata angalau Picha na video Ili kujiridhisha mana upigaji mengi.

Binafsi sishabikii ujinga huu mana unafhalilish sana na hapo hata mungu hawezi kukulipa mema hata kidogo Kwa maana inaonekana hujatoa Kwa moyo.
 
Back
Top Bottom