Juzi nilipita msikiti fulani nikakuta nyomi ya watu wamepanga foleni nikawa najiuliza leo kuna kiongozi gani mkubwa wa dini ametembelea huu msikiti.
Kucheki pembeni nikakuta kuna sheikh kanyuka kanzu safi afu uchebe umejaa kiasi akifumba mdomo wakikuambia kautafute hauupati
Uchebe umepakwa bleach mkono wa kushoto kashika rozali isiyokuwa na msalaba afu mkono wa kulia kabeba Canon yenye lens flani hivi kubwa mara nyingi nimekuwa nikiwaona vijana wa Millardayo wakizishika.
Wakati nimezubaa ndio nikasikia kuwa huyo sheikh anapiga picha hao waliopo kwenye foleni wanaopokea msaada.
Nilipouliza kwanini wapigwe picha wakati hii ni sio taasisi ni dini na haikupaswa kuwa na elements za kuchoreshana, jamaa alinijibu hivi.
Aliniambia wanao fund hiyo misaada ni waarabu wa nje, wao wanatoa kiasi cha pesa ambacho wanawakabidhi viongozi wa msikiti husika ila wanataka kuthibitisha msaada waliotoa umetumika kama walivyotaka. Ndio hapo wanahitaji kuona picha kama uthibitisho
Kwa hiyo wanaopanga hizo foleni hawawezi kuchoreshwa kwenye big screen za umma, bali wataonekana kwa wahusika walio fund hiyo misaada
So unao uchaguzi, ubaki na ustaarabu wako wakugoma kuanikwa kwa waarabu ukaji faitie kivyako kupata hayo mahitaji au ule buyu ujikaushe kwenye foleni afu umuache Millardayo afanye kazi yake