Ni sahihi kuwapiga picha watu wanaopewa msaada kidini?

Sasa hivi wafadhili hawatuamini Wabongo usikute wafadhili wanataka wahakikishe kuwa msaada wao umewafikia walengwa. Wanatujua tabia zetu za upigaji
hiyo ni kweli kabisa, kuna baadhi ya watu huomba misaada kwa ajili ya kuwapa wale wasio na uwezo na baadae huwa hawawapelekei wahusika. Kwa hivyo siku hizi wengi huwa wanapenda wapigiwe picha ili kuona kwa uhakika kama misaada imewafikia walengwa.

Ila sasa huyu aliyeleta hiyo picha humu nae pia hakufanya vizuri.
 
Naona jamaa wanajuta 😃 ila ndio hivyo sasa watafanyaje
 

"Ila sasa huyu aliyeleta hiyo picha humu nae pia hakufanya vizuri"

Nimependa hiyo mistari
 


Yeye sasa ndiye mkosefu kwa kuweka hii picha hadharani humu jf. 🙏🏻🙏🏻🙏🏻✔✔
 
Kweli kabisa stara ni kitu muhimu Sana kwakweli.
Hata kama Mimi nikazam pm kwako unibust hlf unakuja hapa barazani unasema umenibust wallah nitakumaind
Kabisa

Na hiyo sasa ndio MANNI WAL- ADHAA( masimbulizi na maudhi) ambayo inabatilisha sadaka.

"Enyi mlio amini! Msiharibu sadaka zenu kwa masimbulizi na maudhi, kama anaye toa mali yake kwa kuwaonyesha watu, wala hamuamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho..................." (2:264)

Allah atuhifadhi
 

Chief

Asante Sana Kwa kusindikiza na Aya mashallah
 
Ahahaajj

Nimekusoma mkuu
 
Hii picha mpaka kufika hapo ndio katika madhaifu ya hiyo njia ambayo inaonekana kama solution ya kukomesha upigaji.
Sio siri wanawadhulumu hao wasaidiwaji, yaani msaada wa siku moja halafu picha ikivuja kama hivi itasambaa ulimwengu mzima hii sawa kweli?
 
Kudhalilisha watu Kwa mgongo wa dini ndio huku Sasa. Kama unasaidia picha ya kazi gani tena?


Wewe hukumsikia mama Samia akilalamika watu wameweka cha juu kwenye bei ya ndege, hukusikia akiwaita; Pumbavu watu waliochelewesha malipo na riba ikapanda kwa mabilioni ya shillings??-- hao ndio Watz waliokabidhiwa dhamana ya nchi kisheria wanafanya madudu bila kuogopa mkono wa sheria, sasa vipi mtu kajitolea sadaka yake kuwapa maskini, mtu huyo hana mkono wa kisheria juu ya mtu aliyemuamini kwenda kuwapelekea hizo sadaka kwa walengwa?!!--- ni lazima katika mazingira hayo huyo mtoaji sadaka afanye kitu kitakachomridhisha kuona kwamba sadaka yake imewafikia walengwa, hiyo ndio sababu ya hizo picha.
 
Siasa ❌
Dini ✔️
Wachague dini au siasa
 
Inategemea na lengo la anayepiga hiyo picha,Mungu anahukumu kutokana na lengo/nia ya muhusika,picha inaweza kutumika ili kuhamasisha na wengine watoe misaada kwa wenye uhitaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…