Ni sahihi kwa kampuni ya simu kutoa mawasiliano binafsi ya simu kwa umma?

Mmawia

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
122,494
Reaction score
96,074
Nimesikia jana kuwa kampuni moja ya simu imetoa mawasiliano ya Sabaya mahakamani.

Je, hili linatoa taswira gani kwa wateja wake?

Binafsi siijui sheria hivyo nawaomba wenye uelewa tujulishane.
 
TCRA,POLICE,BOT etc wanalindwa na sheria ya kupewa taarifa yeyote wanayotaka kutoka taasis zozote kwa ajili ya uchunguzi.
Ni kweli hilo lipo kisheria kwa kampuni kuwajibika kutoa taarifa kwa vyombo vya uchunguzi ila sio kwa uma wa kawaida.Sheria ya Mitandao EPOCA.huoni hata Maxence Mello wa huku alisumbuliwa kweli na kesi kwa kukataa kutoa taarifa binafsi za members humu
 
Waliogopa kuwakuta ya Mello. Mello ni mwandishi. Kwa kawaida mwandishi kushtakiwa, kupigwa kwake ni jambo la kawaida. Mitandao ya simu wako kibiashara 100% hivyo wanaogopa kufungiwa. Si unaijua Tanzania? Ni maoni yangu tu
 
Nimesikia jana kuwa kampuni moja ya simu imetoa mawasiliano ya Sabaya mahakamani.

Je hili linatoa taswira gani kwa wateja wake?

Binafsi siijui sheria hivyo nawaomba wenye uelewa tujulishane.
Unayaona Leo hayo au?

Sheria zimewekwa kama utaratibu tu unavyotaka, Wanaosimamia sheria ni wale wenye Mamlaka

Katiba yetu imetoa mwanya kuna watu wapo juu ya sheria na huwezi kuwagusa

Hivi Mkurugenzi wa Voda au Tigo ana nguvu gani akitumiwa wale Jamaa, Najua unawafahamu

Maisha yako binafsi ni muhimu kuliko kukumbatia taarifa zinazohitajika na watu waliojuu ya katiba

Kwa usalama wa Taifa au nchi ukigoma kutoa taarifa kesho tunaweza tukakusindikiza kwa nyimbo za pala panda ikilia

Sheria zipo, Kuna muda lazima uangalie maisha yako

Huwezi Shindana na mtu ana Vifaru, Bunduki na Jeshi lote linamuheshimu

Mdomo na kiburi vimewagharimu watu maisha na Leo wameacha familia kisa tu kujifanya wanafuata sheria na katiba

Katiba ni karatasi tu, Wanaosimamia katiba wapo juu ya katiba

Muda wowote sheria hupindishwa au kunyooshwa kwa matakwa ya Mamlaka
 
Waliogopa kuwakuta ya Mello. Mello ni mwandishi. Kwa kawaida mwandishi kushtakiwa, kupigwa kwake ni jambo la kawaida. Mitandao ya simu wako kibiashara 100% hivyo wanaogopa kufungiwa. Si unaijua Tanzania? Ni maoni yangu tu
Ok sasa hapo haki ya siri za mteja inazingatiwa vipi kwenye hali ya uoga ?
 
Mkuu Waswahili husema kwa muoga huenda kicheko, kwa shujaa huenda kilio. Hapa tunapata funzo kwamba tuwe makini katika mawasiliano ya simu. Kumbuka hii Iko hivyohivyo hata kwenye mabenki. Kisheria kuna taasisi zinaweza kuziagiza taasisi hizo kutoa taarifa na wakikataa ni kosa. Inahitaji moyo na taaluma kama ya Mello kuwa jasiri na kusema hapana.
 
Tumpongeze sana mshika dau mwenzetu wa jf
 
Back
Top Bottom