Ni sahihi kwa kampuni ya simu kutoa mawasiliano binafsi ya simu kwa umma?

Nashukuru kwa kunipatia elimu maana elimu haina mwisho.


Soma sehemu inayoonesha mamlaka ya polisi
 
Nimesikia jana kuwa kampuni moja ya simu imetoa mawasiliano ya Sabaya mahakamani.

Je, hili linatoa taswira gani kwa wateja wake?

Binafsi siijui sheria hivyo nawaomba wenye uelewa tujulishane.
Kichwa habari unasema umma, habari ndani inasema mahakama. Kifupi suala likishaitwa la kiuchunguzi halina mipaka tena hasa kwa sheria zetu.
Polisi wanauwezo wa kuomba mawasiliano ya mtu yeyote kwa sababu za kiuchunguzi
 
Kichwa habari unasema umma, habari ndani inasema mahakama. Kifupi suala likishaitwa la kiuchunguzi halina mipaka tena hasa kwa sheria zetu.
Polisi wanauwezo wa kuomba mawasiliano ya mtu yeyote kwa sababu za kiuchunguzi
Nashukuru kwa elimu .
 
Huku kwetu watu ni waoga wanaogopa kufa,kule Marekani kuna tukio moja lilitokea miaka michache iliyopita,kampuni ya apple waliigomea katakata FBI,kuifungua simu iliyowekwa lock,iphone hiyo ilikuwa inamilikiwa na kijana mmoja mwenye asili ya Asia ambaye alishukiwa kwenye tukio la ugaidi,ambapo aliidondosha simu hiyo na makachero wa FBI,walishindwa kuifungua simu hiyo,hiyo simu ilivyotengenezwa ilikuwa ukifanikiwa kuifungua kwa kuilazimisha basi inafuta data zote,kwa hiyo FBI kimbilio lao la mwisho kuifungua simu hiyo ilikuwa ni kuwaomba kampuni ya Apple wawasaidie kuifungua simu hiyo,lakini Apple wakakataa kwa kuhofia Siri za mteja wao zikianikwa basi kampuni yao ingekosa sifa ya kitu za Siri za wateja wao,na jinsi sheria za Marekani zilivyo,FBI hwakuwa na uwezo wa kuilazimisha Apple kufanya upuuzi huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…