Ni sahihi maji ya mvua kutumika kunywa?

Ni sahihi maji ya mvua kutumika kunywa?

Chrix_Tz

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2015
Posts
880
Reaction score
1,100
Kumekua na deaturi ya watu wengi kukinga maji ya mvua pindi mvua inyeshapo, na kufanya kama maji ya kunywa bila kuzingatia usalama wowote wala tahadahari. Mfano labda kuchemsha au kuweka dawa ya maji ili yawe salama zaidi...mie mwenyewe ni muhanga wa hiki kitu... SWALI.. je MAJI HAYO NI SALAMA KAMA TUNAVYODHANI AU KUNA MADHARA YOYOTE TUNAWEZA KUPATA KWA KUTUMIA MAJI YA MVUA?!
 
Hayo ni kwa ajili ya mimea na wanyama p. yetu binaadam yanatakiwa yatoke ardhini kwenye miamba.
Rejea maandiko ya dini.. hakuna nabii aliyeomba maji ya kunywa akashushiwa mvua ila walipatiwa chem chem na visima tuu, jiulize why.? Kwa mara ya pili.

Sent using Jamii Forums mobile app

Huo ni upande wa maandiko tukirudi kisayansi imekaaje hapo? Ni salama au si salama? Maana asilimia kubwa ya watu wanatumia haya maji na hakuna sehem ktk maandiko ilipokataza mkuu....
 
Mm ninachojua hayana chumvi wala magadi ni maji ambayo hayajagusa laana ya ardhi ukinywa ni burudani kabsaaaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app

Ukisoma alichosema huyu jamaa km tukirudi kiimani tunaona alichosem ni hivi
Hayo ni kwa ajili ya mimea na wanyama p. yetu binaadam yanatakiwa yatoke ardhini kwenye miamba.
Rejea maandiko ya dini.. hakuna nabii aliyeomba maji ya kunywa akashushiwa mvua ila walipatiwa chem chem na visima tuu, jiulize why.? Kwa mara ya pili.

Sent using Jamii Forums mobile app
na ww unasema kuwa ni salam kwani hayajagusa ardhi hivyo hayana laana mnanipa mchanganyo kidogo ktk hili...... lipi ni sahihi kati ya haya wakuu???
 
Kumekua na deaturi ya watu wengi kukinga maji ya mvua pindi mvua inyeshapo, na kufanya kama maji ya kunywa bila kuzingatia usalama wowote wala tahadahari. Mfano labda kuchemsha au kuweka dawa ya maji ili yawe salama zaidi...mie mwenyewe ni muhanga wa hiki kitu... SWALI.. je MAJI HAYO NI SALAMA KAMA TUNAVYODHANI AU KUNA MADHARA YOYOTE TUNAWEZA KUPATA KWA KUTUMIA MAJI YA MVUA?!
Maji ya mvua sio salama sana kama watu wanavofikiri kwa sababu;
Moja ni uchafuzi wa mazingira unaoendelea ambapo kuna dust particles either from burning fuels or any other air pollution from industrial emmitted gases zinakua around the atmosphere which contaminate the rain drops as the result maji yanakua sio salama kwa kunywa.. kuna gases nyingine zikiyeyuka kwenye maji ni inivisible but very harfmful to human health.

Pili tunaangalia kitu kinaitwa catchment.. apa catchment tunazungumzia pale ambapo matone ya mvua hutua yakitokea juu..mfano bati tukiongelea katika mazingira ya nyumba. Bati unakuta lina kutu, vumbi na matakataka mengi, mengine majani ya miti ambayo yanaweza kua makazi pia ya vimelea magonjwa hivyo maji yanakua sio salama.

Sasa tunafanyaje ili tupunguze contamination ya haya maji?

Moja ni kuhakikisha bati linakua halina kutu maana kama tunavojua chuma chochote hakitakiwi kwenye mwili wa binadamu.
Mbili, mabati wandugu yasifishwe kabla ya kuvuna maji hasa wale ambao mabati yao yanakua na majani kutokana na mti kua juu ya mabati..
Tatu, mvua kinyesha usikimbilie kukinga maji, subiri kidogo ili maji yalisafishe bati na baada ya muda kidogo ndo ukinge..
Nne, maji ya mvua yanatakiwa kua treated kwa either kuchemsha nyuzi joto 100°C au kuweka chorine kuua vimelea vyovote vya magonjwa.

Nb: Maji ukiyaona ni safi haina maana ni salama kwa kunywa.. kwaio ni vizuri yawe treated ili yawe salama.
Asante!

Asante mkuu kwa maelezo yako kikamilifu hapo nimekuelewa vema [emoji817] nadhan na wadau wengine wanapaswa kusoma na kuelewa hili kwa wale ambap tulikua hatuelewi.....[emoji106] sio vibaya ukapitia pepsi hapo kwa bwana mangi nitakuja kulipia[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Maji yakingwayo kutoka kwenye bati za nyumba huenda yakawa sio salama bila ya kuyachemsha - kwa vile ndege hutua juu ya bati na kuacha vinyesi vyao - hali inayoweza kusababisha magonjwa ya tumbo. Vivyo hivyo kwa vifaa vingine vya kukingia maji.

Kuhusu maji ya mvua kukosa madini fulani fulani - hiyo sio hoja kwa vile watu hula vyakula tele vingine vyenye madini na virutubisho mbalimbali.
 
Hayana madhara yakiwa fresh ila ukiyahifadhi bila cloride kwa wiki mbili au zaidi yanaanza kuteleza.

Na ww unapenda sana mkuu kutumia haya maji inaonekana[emoji16][emoji16] ila nadhan pia usafi uzingatiwe zaid km alivyosema mdau mmoja huko juu en sio salama 100% ukumbuke
 
hayo maji yana acid but ni weak acid, shuhuli za uchafuzi mazingira kama uchomaji taka, viwanda, vumbi na moshi linalopanda juu hushushwa na mvua ...hivyo si salama kwa kunywa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hayo maji yana acid but ni weak acid, shuhuli za uchafuzi mazingira kama uchomaji taka, viwanda, vumbi na moshi linalopanda juu hushushwa na mvua ...hivyo si salama kwa kunywa

Sent using Jamii Forums mobile app

Eh kwahiyo tuyaache kuyanywa sasa mkuu km ni hivyo ni hatari kwahiyo unataka kusema hizo chemically ndio zinashushwa kwa mvua kurudi ardhini?
 
Kumekua na deaturi ya watu wengi kukinga maji ya mvua pindi mvua inyeshapo, na kufanya kama maji ya kunywa bila kuzingatia usalama wowote wala tahadahari. Mfano labda kuchemsha au kuweka dawa ya maji ili yawe salama zaidi...mie mwenyewe ni muhanga wa hiki kitu... SWALI.. je MAJI HAYO NI SALAMA KAMA TUNAVYODHANI AU KUNA MADHARA YOYOTE TUNAWEZA KUPATA KWA KUTUMIA MAJI YA MVUA?!

Mkuu, kitaalamu sio mazuri kuyanywa maji ya mvua.

Kama jinsi wenzangu walivyosema, ni kwamba katika hewa kuna chembe chembe za vumbi na kemikali hasa mahali ambapo kuna viwanda vinavyotoa mioshi pia katika hewa kuna hewa ya carbondioxide ambayo huchanganyika na maji ya mvua pindi inaponyesha mvua na kutengeneza Carbonic acid (weak acid), yaani ni ile hali ya uchachu wa mbali unaouhisi unapokunywa maji ya mvua na hiyo carbonic acid hutoka pindi maji yanapoka kwa siku kadhaa yaani ile carbon dioxide huondoka katika maji kutokana na joto la kawaida (Room temp,) na ndipo maji ukiyatumia kunawa au kufulia huwa yanateleza kwa sababu yanakuwa "soft water" au demineralised,. Ukiachilia mbali hatua na mazingira ya ukusanyaji wa maji ya mvua kiafya, maji ambayo tunashauriwa kiafya tunywe ni "minerised water" (mfano maji ya chupa) ambayo ndanimo kunakuwa na madini yenye faida katika miili yetu na madini hayo kimsingi mengi yanapatikana kwenye udongo (ardhini) hivyo ni muhimu maji ya mvua yakutane kwanza na udongo ili yaji neutralise yanapokutana na kemikali za udongo na hapohapo yachukue madini muhimu kwa afya zetu sisi na mimea pia.

Ukinywa maji ya mvua (pure rain water) PEKEE, ni sawa na kunywa distilled water ambapo yanapoingia tumboni katika utumbo mdogo kuna kitu kinaitwa OSMOSIS Kitatokea kati ya hayo maji na damu, kama tujuavyo ni katika utumbo mdogo ndipo viini, madini, na virutubisho tunavyokula hufyonzwa ili viingie kwenye mfumo wa damu, inapotokea hali hiyo ya kunywa maji ya mvua mengi ni kwamba viini na virutubisho hutolewa kwenye damu kuja kwenye hayo maji hivyo haishauriwi kunywa maji ya mvua mengi pekee bila kula chakula na mboga mboga na matunda.Na ndiyo maana Mungu akaweka mito inayotiririsha maji ardhini, Mungu ni biggest scientist.

Kifupi maji ya mvua si salama kunywa katika hali ya KAWAIDA.
 
Back
Top Bottom