Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,455
- 5,134
Mama mkwe wangu namheshimu sana kama mama yangu ila kitu napishana naye ni pale anapotaka kuingia kuwa mzazi wa watoto wangu.
Ananiingilia sana kwenye malezi, kila nikifanya maamuzi kwa watoto wangu yeye anapingana nayo anataka mtoto alelewe vile yeye anaona inafaa mpaka nashindwa kuelewa huyu mama anajiona ndio mlezi sana au vipi au anajikuta nani.
Nikinunua vitu kwa ajili ya watoto wangu anasema nawadekeza watoto, sijui nacheka sana na watoto, watoto hawatakiwi kuona wanajaliwa watakuwa wazembe yaani ananichosha.
Anajisifia kuwa yeye watoto wake walikua na adabu mtaa mzima ila wangu hawana adabu kisa malezi yangu, anasahau naishi na mtoto wake na hizo abdabu sizioni.
Ma mkwe wangu ananichosha hapo tu badala aniache nilee watoto wangu kwa namna nayo taka mimi yeye anataka niwalee kama enzi za mkoloni, hataki mtoto ahoji, aongee eti mtoto hawezi muhoji mtu mzima, namwambia hiyo ndio sababu mpaka sasa tunateseka hatujui kujieleza kisa tulinyimwa fursa utotoni, anaona nakosea.