Ni sahihi mwanamke kumkosoa mume wake/boyfriend?

Ni sahihi mwanamke kumkosoa mume wake/boyfriend?

Na hapo kwenye lugha? Nitumie njia gani kumrekebisha asione kama namletea dharau na kujiona ni msomi kuliko yeye?
Km kuna ulazima wa kumrekebisha “it sounds better..”.....................” Nashaur ingekuwa “.....,.......................” kwa mm ningechkulia Poa ila km Upo na mpenda sifa ni busara kukausha tu
 
Na hapo kwenye lugha? Nitumie njia gani kumrekebisha asione kama namletea dharau na kujiona ni msomi kuliko yeye?
Type kirengeza kwanza tujue kama unajua....usikute nawe unachapia balaa halafu unajitia ujuaji kukosoa.


Utafsiri huo mchango wangu kwa kizungu.
 
Ishu sio Kukosoa au Kukosolewa

Ishu ni ile Inner Tone ya Kukosoa.
 
Ila kiukweli kabisa kuwa mwanaume Ni Raha kinoma, Embu fikiria kama usingekua Dume Muda huu ungekua unashikwa shikwa makalio na wahuni.
 
Nilimwambia "babe lini hiyo, sio kwamba uchaguzi bado?"
akaniambia "upo dunia gani wewe, ameshatangazwa kuwa Rais kabisa".
nikamuuliza "mbona hata BBC Swahili hawajatangaza beb.
Akaniambia '' niamini mimi, hao bbc walikuwa vibaraka wa Trump hawawezi kutangaza."
Nikamwambia "sawa baby wewe umeona wapi"
Akanitumia screenshot ya facebook, ni kweli imeandikwa hivyo lakini na page za uongo.
Akaniuliza "umeamini sasa ?'
Nikamjibu "ndio hongera yake"
Sasa roho inaniuma kiasi kwamba naona ataenda kuongea mbele ya watu kwa ujasiri aonekane kichekesho. Na ningemthibitishia kwa kumwonesha source sahihi angeona namwona kilaza. Na kwa maoni niliyoyapata hapa naona nilifanya uamuzi sahihi wa kuacha aamini hivyo.
Aiseee kuwa na mwanaume kilaza ni mtihani sana

muache wakamcheke vizuri atajifunza
 
Sasa unamcheka nini! Si unamwelewesha tu yanaisha.
Sio mimi kumcheka...ni dhana inayoonekana kuwa mwanaume hakosei kitu ambacho sio kweli

Binafsi huwa sipendi kusahihisha sana watu sio mwanaume tu

naweza nkasema fact bila kukuhusisha wala kukusahihisha hapo hapo
 
Yani simple fact kama ya Biden kuwa ni nominee na sio Raisi unaanzaje kumuelewesha mtu?

mana mjuzi yoyote wa mambo anajua uchaguzi wa US huwa ni November..

Kuna vitu ni vya kuacha tu esp km mtu anajiona mjuaji..ipo siku atakutana na wabishi zaidi yake watamuweka sawa!
 
wewe umpe dyudyu tu.....kakosoe wanao.....mwanaume hakosolewi,,,,usiivuruge ndoano yako
 
mimi huwa namkosoa mamaa kwa kumcheka. natumia ucheshi nisionekane namuumbua, namdharau au najifanya mjuaji.
basi na yeye anaishia kucheka utamskia niskosee kwani mi Malaika, au baby tuwe serioud bwana!

kuna ripoti nilikua namsaidia kuandika sasa kiingereza chake kinachekesha haswa na akaniambia nimsaidie kurekebisha huku akisisitiza nisimcheke, mi nkashindwa kuvumilia asee.

ila baada ya hapo maisha yanendelea kama kawaida. na ikitokea kesho kachapia namcheka tena.
 
Back
Top Bottom