Ni sahihi mwanaume kupaka manukato yenye kunukia sana?

Ni sahihi mwanaume kupaka manukato yenye kunukia sana?

Expensive life

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2020
Posts
2,971
Reaction score
9,437
Habari Wana JF

Huu mjadala nimeukuta mahali, nikaona ni vyema nikauleta huku nishee mawazo yenu.

Ni sahihi mwanaume kupaka manukato yenye kunukia sana?

Ni sahihi mwanaume kuoga mara tatu kwa siku?

Kwa upande wangu mimi haya manukato yamenikaa mbali.

Kila binadamu iwe ke/me ana uhuru wa kuchagua kile anacho kipenda, jamii zetu zimekuwa tofauti kidogo wapo wanaodhani anayestaili kunukia ni mwanamke tu.

Iwapo akipita mwanaume anayenukia humchukulia tofauti.
 
Mwanaume unaogaje Mara 3 umekua mwali wahuni wenyewe ratiba ya kula Milo mitatu ni muhimu lakini tulishaivuruga tukila sana tunakula milo miwili tu
milo miwili ili iweje mkuu
kula mlo mmoja unatosha, labda kama wewe ni mkulima, hapo sawa kula hata mitatu
 
Mwanaume unaogaje mara Tatu,
Mnaoga oga sana shenzi nyiiie
Kama kuonga ingekuwa ni usafi mbona Samaki inanuka.,
Nyie ndo mnasababisha mgao wa dawasco

Alisikika kijana mmoja
 
Ili iweje Sasa umekuwa jini wewe..? Mwanaume unatakiwa kunukia ugali ugali fulani hivi..😂
 
Mwanamke anukie na Mwanaume pia anukie?

Me wa kibantu anatakiwa anukie ukwapakwapa kuwasilisha harufu ya ubeberu A.K.A mbuzi dume[emoji123]
 
Inasemekana wanawake wanapenda harufu nzuri ya kunukia, ivyo mwanaume anaponukia kwa harufu nzuri zaidi huwavutia baadhi ya wanawake huonekana nadhifu zaidi kwao
NB: sijafanya utafiti wowote
 
Mkuu, wanawake hawajawahi kueleweka wanataka nini.
Inasemekana wanawake wanapenda harufu nzuri ya kunukia, ivyo mwanaume anaponukia kwa harufu nzuri zaidi huwavutia baadhi ya wanawake huonekana nadhifu zaidi kwao
NB: sijafanya utafiti wowote
 
Tafuta hela brother, sauvage dior au invictus by paco rabanne ni zaidi ya 250K 100mls, dont hate players hate the game.
 
Back
Top Bottom