Ni sahihi mwenye nyumba kumwekea mpangaji sharti la aina ya wageni wanaomtembelea?

Sasa wasiwe wengi inakuwa kero bana!!
Unakuta na midada mingine ina misifa inapiga mikelele ya sauti za kimahaba mnaanza kutesa wengine kihisia 🤣
 
Unda Teeth yako binafsi, imfuatilie huyo Mzee ni Dini/Dhehebu gani?. Kuna madhehebu wachumba kuonana hadi awepo mtu wa tatu[emoji1787]
Wewe utakua dishi limeyumba sio bure,unaonekana ni mtu mwenye umri mkubwa ila kichwani patupu,

Hii mada haihusiani na udini,tutolee upuuzi wako hapa.
 
Kuna mwenye nyumba wengine hasa wa kike wao huomba omba vyakula kwa wapangaji wao kuanzia asubuhi mpaka usiku. Wanaishi kwa kugongea misosi kwa wapangaji wao. Ukiwa msela tu huna mke na hupiki geto ataomba hela ya kitunguu, nyanya, chumvi, kiberiti na vikorombwezo vingine. Ni kero tupu
 
wanajiamini sana kiasi cha kupangia wapangaji masharti ya kuishi. Unapangiwa namna ya kutumia choo na kujisafisha utumie material gani, muda wa kurudi usiku, aina ya vyakula vya kupikwa, muziki wa kuwekwa na aina ya wageni wa kuja
Imagine mtu ukikubali kuishi namna hiyo kwa miaka mitatu tu utakuwa umepoteza kiasi gani cha maisha yako. Si jambo jema kwa afya ya akili na ustawi wa mwanadamu.
 
Njoo uku kwetu mwenye apartment ana namba za malaya wa levo zote ukiwa mpangaj mnyonge mnyonge anakwambia hapa n olmpk utapaweza kwel
 
Mimi nilipata changamoto mwanzoni baada ya siku kupita nikala kuku na mayau yake
 
Mimi niliambiwa siruhusiwi kulala na watu zaidi ya 3 Yani kama ndugu zangu wamenitembelea wengi hawaruhusiwi😭
 
Ni vizuri kuwe na utaratibu wa wageni,kwani si ustaarabu kugeuza chumba kuwa DANGURO,lakini vilevile wakati mwingine haohao wageni huwa ni WEZI,
 
Sasa wasiwe wengi inakuwa kero bana!!
Unakuta na midada mingine ina misifa inapiga mikelele ya sauti za kimahaba mnaanza kutesa wengine kihisia 🤣
Hapo kwenye kelele nakubali kuwa ni kukosa ustaarabu kwenye eneo ambalo watu wanaishi kama jumuiya. Lakini kama hakuna hayo au matusi na mambo mengine ya ajabu yanayotokea, basi mwenye nyumba hapaswi kuleta tu hisia za kwamba kuna ngono inaendelea humo ndani. 😂
 
sema ulikua unabadilisha mademu wa kila sampuli si wageni wa kike.

sema nini ?

kuna vojana mna mambo ya hovyo hovyo kweli mkipanga sehemu panageuka kua dangulo yaani wanawake wanapishana kama clinic vile tabia ambayo sio ya kistaraabu kabisa.

sina nyumba mjini hapa ila nikijenga halafu nikapangisha kijana akawa na mambo ya hovyo hovyo kama wewe nakuondoa chap.

ndio maana sehemu zingine ukienda kupanga swali la kwanza ni UMEOA ?

ili kuepusha mambo ya aibu kwenye mji.
 
tunaijua hio 😁
 
Hata mm nikijenga nyumba yangu siwezi ruhusa kuwa sehemu ya kufanyia uzinzi, kama ninge taka kujenga sehemu ya kufanyia uzinzi ninge jenga guest bubu.
 
Hata mm nikijenga nyumba yangu siwezi ruhusa kuwa sehemu ya kufanyia uzinzi, kama ninge taka kujenga sehemu ya kufanyia uzinzi ninge jenga guest bubu.
Natumai umesoma na kuelewa hoja yangu.
 
Kuna mwenye Nyumba mmoja mkataba wake ameandika wageni wakija kumtembelea mpangaji wasikae zaidi ya siku moja maana watajaza Choo.
Hiyo ni sahihi kabisa kwasababu nyumba inapojengwa kwa mfano apartments hujengwa kuzingatia jumla ya watu watakaoishi humo ; ndio maana kabla ya kupangishwa unaulizwa ukubwa wa familia yako ili iendane na capacity ya nyumba husika.
Wenyenyumba wasipokuwa strict kwa mfano apartment ya vyumba viwili mpangaji anaweza kuleta ndugu zaidi ya sita kuishi humo! Hii si busara kwani sio tu nyumba its jamaa upesi bali pia sio vizuri kwa afya za wahusika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…