Mayu
JF-Expert Member
- May 11, 2010
- 7,621
- 12,505
Imagine wewe ndio mmiliki wa Azam TV halafu unasikia TBC wanaonesha bure michuano mikubwa ya CAF CHAMPIONS LEAGUE tena kupitia kisumbusi chako hicho hicho ambacho wewe una wataka watu walipie elfu 24 kuona mechi hizo!
Kibiashara limekaaje hili? Ingekuwa wewe ndio mmiliki wa Azam TV ungefanya nini?
Anauliza mdau kutoka X.
Na declare interest kabisa ninamiliki vibanda umiza kadhaa
TBC ni wapuuzi sana aisee
Wanafanya upuuzi kwa mgongo wa kusaidia “masikini” wakati huo wanaumiza wawekezaji wadogo wadogo wenye vibanda umiza
Walianza na AFCON badala ya kupata maokoto kwenye vibanda vyetu tukaishia kupata hasara tu kwasababu inaonyeshwa bure majumbani hata usipolipia kisumbuzi
Masikini hasaidiwi kwenye STAREHE anasaidiwa kwenye mambo ya msingi
Nimegharamika kujenga banda, viti, Tv, umeme, kifurushi cha kisimbusi na nalipa na kodi nalipa ili nionyeshe mpira nipate maokoto halafu Tv ya taifa inaanza kuonyesha mpira huo bure....... Ntafanya biashara gani sasa