Ni sahihi TBC kuonyesha michuano ya CAF Champions League?


Na declare interest kabisa ninamiliki vibanda umiza kadhaa

TBC ni wapuuzi sana aisee
Wanafanya upuuzi kwa mgongo wa kusaidia “masikini” wakati huo wanaumiza wawekezaji wadogo wadogo wenye vibanda umiza

Walianza na AFCON badala ya kupata maokoto kwenye vibanda vyetu tukaishia kupata hasara tu kwasababu inaonyeshwa bure majumbani hata usipolipia kisumbuzi

Masikini hasaidiwi kwenye STAREHE anasaidiwa kwenye mambo ya msingi

Nimegharamika kujenga banda, viti, Tv, umeme, kifurushi cha kisimbusi na nalipa na kodi nalipa ili nionyeshe mpira nipate maokoto halafu Tv ya taifa inaanza kuonyesha mpira huo bure....... Ntafanya biashara gani sasa
 
tulia we bepari mpevu, mlizoea kuumiza wananchi wasio na kitu mkiwakamua mtakavyo. Endeleeni kuwaumiza kwenye ligi kuu na epl huko nako muda utafika mtapigwa chini mkafanye biashara zingine
 
Nyie wajinga mlioanza kuangalia tv wakati wa azam ni matutusa sana
 
tulia we bepari mpevu, mlizoea kuumiza wananchi wasio na kitu mkiwakamua mtakavyo. Endeleeni kuwaumiza kwenye ligi kuu na epl huko nako muda utafika mtapigwa chini mkafanye biashara zingine

Imebidi nicheke peke yangu tu badala ya kukasirika [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Kiingilio 500 tu [emoji23]
 

Mkuu tatizo hapa sio leseni ya kurusha matangazo

Tatizo hapa ni kulazimisha TBC irushwe kwenye visimbusi vyote BURE
Kifurushi kikiisha TBC inalazimishwa iendelee kuonekana
Na kibaya zaidi inaanza kuonyesha vipindi vya kibiashara ambavyo ndio vinafanya mtu alipie kisumbusi kuangalia
Kifurushi kikiisha mtu hana ulazima wa kulipia tena maana anajua atangalalia CCL buree kupitia TBC

TBC ingejikita na habari za kuelimisha jamii kama Voice of America nk au iwe ya kibiashara kama BBC entertainment
Au waanzishe TBC Burudani ambayo itakua kibiashara na iwe kwenye kifurushi cha kulipia

Na hapo bado wanatuumiza wawekezaji uchwara wa vibanda umiza.... tulipishana na maokoto ya Afcon na sasa CCL
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…