Ni sawa kwa mjamzito kunyimwa huduma za kuanza kliniki kisa hajaambata na mumewe?

Mkono mtupu haulambwi..
Penyeza ka rupia.

Lkn ukitaka kufata utaratibu utatakiwa uje na barua ya mwenyekiti wa mtaa.

Tofaut na hapo nenda kaanze clinic kwenye private hosp. Wao wanaangalia noti
Kuna mahudhurio zaidi ya matatu,mume anaweze kuambatana na mkewe kwenye hudhurio lolote.Eti barua ya mwenyekiti wa mtaa,utaratibu huo umeanishwa wapi?
 
Hili jambo limeanza miaka ya 2016 nadhani.

Kutokana na changamoto ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto, kumekuwa na kampeni isiyo rasmi ya kuhakikisha Wazazi watarajiwa wanahudhuria Kliniki kwa pamoja kwaajili ili kupewa Elimu hii.

Kumbuka Baba anaweza kumwambukiza Mama hivyo naye kuja kumwambukiza Mtoto aliye tumboni.

Mkienda kwa Pamoja Kliniki mtapewa Elimu kuhusu umuhimu wa kuendelea kujilinda ili kutomwambukiza Kijacho wenu.

Kama mtakuwa mna maambukizi Mama Kija ataanza atapewa vidonge vya kumlinda Mtoto akiwa tumboni hata atakapo zaliwa.

Ni dhambi Kumwambukiza kwa makusudi Mtoto wenu kwa sababu ya starehe zenu.

Ukiona huwezi kuwa mwaminifu kwa mwenzio ambaye ni Mjamzito, basi hakikisha ukichepuka huko Nje unatumia Kondomu kwa kila tendo tena kwa usahihi.
 
Mnapimwa magonjwa ya zinaa nk. ili kumlinda/kumkinga mtoto.

Mleta mada aende kituoni, au kama yupo mbali aji commit aende hata hudhurio moja.

Vijana waache janja janja ili tupate kizazi bora chenye afya nchini kwa miaka ijayo.
Mnapima baada ya kupeana mimba....mm nazan mpime before
 
Kwenda si
Mnapimwa magonjwa ya zinaa nk. ili kumlinda/kumkinga mtoto.

Mleta mada aende kituoni, au kama yupo mbali aji commit aende hata hudhurio moja.

Vijana waache janja janja ili tupate kizazi bora chenye afya nchini kwa miaka ijayo.
Kwenda si tatizo.tatizo je ni halali kunyimwa huduma elewa hoja.
 
Habari wanajukwaa,

Ni halali mjamzito kukosa huduma kisa hajaenda na mume wake?

Nilitaka kuweka clip nimeshindwa.

Mawazo yenu muhimu.
Ni muhimu wote mume na mke kuhudhuria kliniki haswa kwa first visits kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya awali haswa blood grouping ya wote mume na mke ili kuangalia Rhesus factors zenu kama zina match kusudi kuu kukiokoa kiumbe kisife (Antibody & Antigen reaction ) , pia kwa ajili ya kupima virusi vya ukimwi ili kupewa counselling na huduma muhimu ili kumuondoa kwenye hatari ya mtoto naye kupata maambukizi (PMTCT).
 
Alafu huu mtindo wa kuambatana na mke clinic as if wote mnaenda kupimwa mimba ufe kabsa...
Hiyo kwa manufaa ya huyo mtoto atakayezaliwa kinyume na hapo msishangae kila mimba anayobeba kuharibika mpaka muhisi amerogwa
 
Zahanati ya mshangano manispaa ya songea
Kutakuwa kuna shida. Siyo lazima mama mjamzito aende na mumewe.
Mazingira ya mwanamke kupata mimba ni mengi sana mfano
1. Kwa mfano mtu aliyebakwa, huyo mwanaume atamtolea wapi?
2. Mwanaume kaweka mimba, kaikataa, huyo mwanamke atamtolea wapi mwanaume?
3. Mwanamke anafanya kazi dar na mwingine kagera. Kulingana na ufinyu wa muda, atafunga safari aende dar kwa ajili ya kliniki?
4. Kuna mwingine, mpenzi wake yupo Marekani, amekuja kumtembelea wakakutana kimwili, mwanaume ameondoka ameenda Marekani. Unategemea tena mwanaume aje kwa ajili ya kliniki?
Na mengineyo
Mimi ni shuhuda, naandika kwa kile nilichoona. Anaulizwa majina ya mtu wake tu, matibabu mengine yanaendelea.
 
Kwenda si

Kwenda si tatizo.tatizo je ni halali kunyimwa huduma elewa hoja.
Si halali. Aende kwa mganga mkuu, akashitaki.
Ni haki ya kila mama mjamzito kupata huduma ( Ni lazima wa siyo ombi).
Nimeona kwa zaidi ya wanawake wawili 2016 na 2023 mwezi wa 4, alienda bila mumewe na amepatiwa huduma kama kawaida.
 
Ni muhimu wote mume na mke kuhudhuria kliniki haswa kwa first visits kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya awali haswa blood grouping ya wote mume na mke ili kuangalia Rhesus factors zenu kama zina match kusudi kuu kukiokoa kiumbe kisife (Antibody & Antigen reaction ) , pia kwa ajili ya kupima virusi vya ukimwi ili kupewa counselling na huduma muhimu ili kumuondoa kwenye hatari ya mtoto naye kupata maambukizi (PMTCT).
Kwahiyo ni sahihi kutompa huduma mama mjamzito ikiwa hajaambatana na mume wake?
 
Si halali. Aende kwa mganga mkuu, akashitaki.
Ni haki ya kila mama mjamzito kupata huduma ( Ni lazima wa siyo ombi).
Nimeona kwa zaidi ya wanawake wawili 2016 na 2023 mwezi wa 4, alienda bila mumewe na amepatiwa huduma kama kawaida.
Seems unapenda sana case,,, msisitizo ni kwenda kushitaki siyo? na siyo kuwaeleeza watoa huduma juu ya changamoto iliyomfanya asifike na mwanaume, So far hakuna ambaye atakataa kutoa huduma kwa sababu hiyo ndogo.

Effect za kushitaki watoa huduma zina cost yake "negligence" watakukalili next time watakufanyie kitu hutojua imekuaje .
Hawa watu ni kuongea nao tuu, hizo mbwembwe za kushtakia ziwe last resort kabisa
 
Habari wanajukwaa,

Ni halali mjamzito kukosa huduma kisa hajaenda na mume wake?

Nilitaka kuweka clip nimeshindwa.

Mawazo yenu muhimu.
Usilete siasa kwenye Matibabu .akanyooshe Maelezo ukileta lugha za ukakasi akapime kituo kingine Tanzania kubwa sana vituo ni vingi
 
Ni muhimu wote mume na mke kuhudhuria kliniki haswa kwa first visits kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya awali haswa blood grouping ya wote mume na mke ili kuangalia Rhesus factors zenu kama zina match kusudi kuu kukiokoa kiumbe kisife (Antibody & Antigen reaction ) , pia kwa ajili ya kupima virusi vya ukimwi ili kupewa counselling na huduma muhimu ili kumuondoa kwenye hatari ya mtoto naye kupata maambukizi (PMTCT).
Hii ndiyo sababu ya kunyimwa huduma?
 
N
Seems unapenda sana case,,, msisitizo ni kwenda kushitaki siyo? na siyo kuwaeleeza watoa huduma juu ya changamoto iliyomfanya asifike na mwanaume, So far hakuna ambaye atakataa kutoa huduma kwa sababu hiyo ndogo.

Effect za kushitaki watoa huduma zina cost yake "negligence" watakukalili next time watakufanyie kitu hutojua imekuaje .
Hawa watu ni kuongea nao tuu, hizo mbwembwe za kushtakia ziwe last resort kabisa
Akubaliana nawe.ila ikitokea kwa mambo ya nyuma wanaofanya visa kea mhudumiwa hapo ndiyo pamoto.
 
Back
Top Bottom