Ni sawa Wasanii kutoa ngoma za "ku-party" wakati Profesa J yuko hoi Muhimbili?

Ncha Kali

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2019
Posts
15,335
Reaction score
29,114
Hii imekaaje?

Hili ni swali ambalo mwanangu huyu mdogo kaniuliza, kwa muda nimekuwa nikimsimulia kuhusu HipHop na kumwaminisha kuwa ni muziki wa maisha halisi na mara nyingi huhimiza upendo.

Basi leo yamenishuka, sijui kaniotea vipi.

Ni hivi:
Kina AY na Fid Q tunaweza kusema ni kizazi kile cha Profesa Jei.

Wakati huu mwenzao yupo hoi kitandani kupigania afya yake, hawa wengine wote kwa pamoja wametoa 'Club Bangers'. Kwanza sio watu wa kutoa ngoma kila wakati, kwanini muda huu?

Na mbona isiwe nyimbo fulani za majonzi au faraja kwa lijendi mwenzao?

Dogo kaniacha na maswali mengi, binafsi imenistua.

Get well soon Jay, Mchawi wa rhymes Mti Mkavu.
 
Mkuu maisha mengine lazima yaendelee ndio mfumo
 
Duu kwa hiyo kama akilazwa mwaka mzima ina maana mwaka wote wote watoe nyimbo za huzuni.

Huyo baba taifa Mwl Nyerere kipindi anaumwa kalazwa watu walikuwa wanatoa nyimbo za kuparty kama kawa acheni lawama za kijinga.
 
Sidhani kama uko fair kwa hao Wasanii, ugonjwa wa Prof J ingawaje inasikitisha lkn Dunia haiwezi kusimama kwa ajili yake, wanaopaswa kufanya hayo unayoyataka ni Familia yake yeye J na siyo kila mtu.

Kila la Heri na augue pole!
 
Watoe ngoma wasitoe, hatujasikia kwenda kumjulia Hali, karibia wasanii wote.
 
Mwanao ana umri gani? Ameanza lini kuskiza wakina sugu na fid? Amejuaje hao ni kizaz cha J? Mwanao anajua kua kufa kwa imamu sio mwisho wa ibada? Kifupi Hilo swali sio la mtoto mdogo...

Ukiacha umri, huyu mtoto ana akili kubwa kukuliko.
 
Maisha lazima yaendelee
 
Watoe ngoma wasitoe, hatujasikia kwenda kumjulia Hali, karibia wasanii wote.

Kumjulia hali huenda wanaenda, kama inaruhusiwa…. hiyo sio lazima waposti.
 
Ulifikiria sana ya maisha.. utaumiza kichwa.. maisha kawaida yanaendelea kwa wengine.. labda tu kama mgonjwa alihusika ndio wangemsubiri.. ila yote pia utegemea.

Umepata kusikiliza 'Young Love' ya Fid Q?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…