Ni sawa Wasanii kutoa ngoma za "ku-party" wakati Profesa J yuko hoi Muhimbili?

Ni sawa Wasanii kutoa ngoma za "ku-party" wakati Profesa J yuko hoi Muhimbili?

Mkuu labda unashindwa kuelewa kwa sisi hadhira mziki ni starehe na viburudisho,lakini kwa wasanii ni kazi au ajira.Ni sawa we uache kufanya kazi ya kukuingizia kipato kisa mfanyakazi mwenzako anaumwa kalazwa.

Wasanii makini hutoa ngoma zenye maudhui kuendana na nyakati, mbona wakati mwenzao anapigania roho yake wao wanatoa club bangers.!
 
Hii imekaaje?

Hili ni swali ambalo mwanangu huyu mdogo kaniuliza, kwa muda nimekuwa nikimsimulia kuhusu HipHop na kumwaminisha kuwa ni muziki wa maisha halisi na mara nyingi huhimiza upendo.

Basi leo yamenishuka, sijui kaniotea vipi.

Ni hivi:
Kina AY na Fid Q tunaweza kusema ni kizazi kile cha Profesa Jei.

Wakati huu mwenzao yupo hoi kitandani kupigania afya yake, hawa wengine wote kwa pamoja wametoa 'Club Bangers'. Kwanza sio watu wa kutoa ngoma kila wakati, kwanini muda huu?

Na mbona isiwe nyimbo fulani za majonzi au faraja kwa lijendi mwenzao?

Dogo kaniacha na maswali mengi, binafsi imenistua.

Get well soon Jay, Mchawi wa rhymes Mti Mkavu.
Kwa hiyo na akifa waache muziki kabisa sio? Haya maisha omba Mungu usiwe masikini na uwe na roho ya korosho unaweza kununua uchawi hivihivi bwana mdogo
 
The fact that you don't eat a lion it doesn't act as a bar for the lion not to eat you youngman. Keep your head up, this is a gang world there's no place for the innocent.

The world is full of wickedness, maisha yanasonga brotheman he akifa hela itatoka wapi ya kusaidia mazishi? Hela lazima iendelee kutafutwa ndio maana siku hizi hata duka la mtaani kwenye msiba tunawaambia asifunge maana ndio tutapata huduma hapo.

It's not Armageddon, life has to go on.
 
Wanatakiwa watoe hata wimbo mmoja wa kumpa faraja mwenzao. Huo wimbo Jay akipona atausikiliza na kuongeza umoja zaidi.
Sio kusubiri sijui mambo gani ndio wajifanye wanajua kupangilia vina kwa nyimbo ambazo mhusika hatasikiliza.
 
N wangap wanalazwa na maisha yanaendelea, wacha hzo fkra. Maisha n lzma yaendelee.

Hatupangwingwiiii 🤣🤣
 
N wangap wanalazwa na maisha yanaendelea, wacha hzo fkra. Maisha n lzma yaendelee.

Hatupangwingwiiii [emoji1787][emoji1787]

Sikiliza wimbo wa Profesa Jei, msinitenge…. alishasema yote humo.
 
Huwezi kusimamisha kazi zako kwa sababu mtu uliyenaye kwenye industry moja anaumwa, mfano ni waalimu na mwenzenu mmoja anaumwa tena kwa muda mrefu hamtaendelea kufundisha? Siku hizi hata jirani yako akiwa na msiba na wewe unakiduka chako hapo, huwa hawafungi na akifunga tu ni pale anaenda kuzika. Watu wamejiajiri na wana watu nyuma wanamtegemea, aache kufanya kazi kwa sababu fulani kalazwa!
 
Ikitokea msiba kwa jirani ukapiga sebene hutoeleweka, utapiga nyimbo fulani kama kwaya.
Hivyo, hata hawa wangetoa nyimbo zenye maudhui ya faraja na kutia moyo kuonesha umoja.

Huo ndio upendo wa kweli.
 
Back
Top Bottom