Mkuu labda unashindwa kuelewa kwa sisi hadhira mziki ni starehe na viburudisho,lakini kwa wasanii ni kazi au ajira.Ni sawa we uache kufanya kazi ya kukuingizia kipato kisa mfanyakazi mwenzako anaumwa kalazwa.
Kwa hiyo na akifa waache muziki kabisa sio? Haya maisha omba Mungu usiwe masikini na uwe na roho ya korosho unaweza kununua uchawi hivihivi bwana mdogoHii imekaaje?
Hili ni swali ambalo mwanangu huyu mdogo kaniuliza, kwa muda nimekuwa nikimsimulia kuhusu HipHop na kumwaminisha kuwa ni muziki wa maisha halisi na mara nyingi huhimiza upendo.
Basi leo yamenishuka, sijui kaniotea vipi.
Ni hivi:
Kina AY na Fid Q tunaweza kusema ni kizazi kile cha Profesa Jei.
Wakati huu mwenzao yupo hoi kitandani kupigania afya yake, hawa wengine wote kwa pamoja wametoa 'Club Bangers'. Kwanza sio watu wa kutoa ngoma kila wakati, kwanini muda huu?
Na mbona isiwe nyimbo fulani za majonzi au faraja kwa lijendi mwenzao?
Dogo kaniacha na maswali mengi, binafsi imenistua.
Get well soon Jay, Mchawi wa rhymes Mti Mkavu.
Kafa jembe langu magufuli na bado John nimebaki kunywa pombe na kugarauka
#Kazi IendeleeMaisha ni lazima yaendelee!
Huwezi kusimamisha kazi zako kwa sababu mtu uliyenaye kwenye industry moja anaumwa, mfano ni waalimu na mwenzenu mmoja anaumwa tena kwa muda mrefu hamtaendelea kufundisha? Siku hizi hata jirani yako akiwa na msiba na wewe unakiduka chako hapo, huwa hawafungi na akifunga tu ni pale anaenda kuzika. Watu wamejiajiri na wana watu nyuma wanamtegemea, aache kufanya kazi kwa sababu fulani kalazwa!