Ni sehemu gani Dar affordable kuanzisha maisha ukiwa na familia yako?

Ni sehemu gani Dar affordable kuanzisha maisha ukiwa na familia yako?

Mtu Yuko serious alafu watu wanaleta masihara jamiiforum pamekua sehemu pa mzaha na masihara ya kitoto sio sehemu ya kupata msaada
Umeshasema jamii hapo tegemea watu wa aina zote vichaa, wendawazimu, mazuzu, majini, wachawi, wenye akili timamu, wachamungu, matapeli nk, nk
 
Inategemea na mishe mishe zako! Kama wewe ni fundi ujenzi basi chagua kukaa pembezoni mwa mji ndipo gharama za maisha zipo chini...Kama umeajiriwa ofisi town basi kaa Mbezi ya Kimara.
 
Kama huna shughuli maalumu kama ajira ya kukufanya lazima uishi sehemu fulani karibu na kazi yako.. nakushauri nenda yombo buza na maeneo jirani na huko sababu vyumba bei rahis na nyumba bado hazijachoka zina upya upya na usafiri kwenda sehemu nyingi za muhimu dar ni bus moja tu. Ama nenda kitunda pia napo ni hivyo hivyo.. pia manzese na tandale maisha ni nafuu ila changamoto yake nyumba zake ni za zamani bati full kuvujaaa na mitaa hailali usiku
Kuliko kukaa hayo maeneo Bora nikakae mkoani
 
Wanandugu ninataka wa kuanzisha maisha nikiwa na familia yangu nikiwa na mke wangu na pamoja na mtoto wangu

Hivyo ningependa kufahamu ni sehemu gani hapa Dar kuanzisha maisha ambapo ninaweza kupanga vyumba viwili at affordable price na eneo nitakaloishi lisiwe la gharama hivyo naomba kufahamu ni wapi nitaanzia maana mwanamke wangu saivi ana ujauzito hivyo nataka kumtoa kwao nianze kuishi nae
Affordability ni function ya uwezo wako kifedha
 
Tandale ama Buguruni ila uwe na ujasiri wa kukabiliana na Uswahili. Ukienda maeneo mengine utajuta. Tandale ni karibu na Posta na Muhimbili ni sawa na Buguruni ilivyokaribu na Kariakoo na Posta na Muhimbili. Urahisi wa maishi ni kutokana na vitongoji hivi kuwa na masoko ya vyakula sawa na bure. Pia Buguruni kuna huduma ya kupona hamu ya ngono kirahisi na gharama ipo chini sawa na Tandale Uwanja wa Fisi.
 
Mh bomba2 usipende utajuta sana msimu wa mvua, magari hayafiki huko halafu barabara zote zimejaa maji kama si kupata chemchema ndani ndani ya nyumba
Inategemea na mishe zako unafanyia wapi.

Angalia sana eneo ambalo kwenda kazini haikulazimu upande gari. Kama unataka bei rahisi ya kumudu panga nyumba isiyo na umeme, zipo nyingi sana katikati maeneo ya Magomeni, Ilala Bomba, Mchikichini, ila tu hakikisha kuwa maeneo hayajai maji kipindi cha mvua, ni rahisi kujua maeneo yanayojaa maji na kufurika.

Vyumba ni kuanzia 25000 kama hakina umeme, mimi ninasubiri kumalizia nyumba yangu nimepanga sehemu haina umeme hapa Magomeni Mapipa kwa 35000 na ninafurahia maisha ninayoishi na familia ya mtoto mmoja.

Kama unahitaji nitafute nikuoneshe vyumba vizuri vya bei hiyo niliyotaja na mahali ambapo hamna usumbufu.

Utafunga sola ya mkopo wa ZOLA kila mwezi unalipa 10,000 kwa miezi 14. Sola yao inachaji simu mbili kwa siku pamoja na kuwasha taa tano, ila ukitumia taa mbili zinatosha sana.
 
Swali lako ni mtambuka kwa kuwa kuishi maisha affordable kuna factor nnyingi za msingi kuangalia. Mathalani unaweza kupata nyumba ya bei rahisi kupanga ila gharama za maisha kwa maana ya nauli na mahitaji mengine ya muhimu ikawa juu.
Kwa mantiki hiyo ni lazima tufahamu aina ya shughuli zako ili tukushauri accordingly!
 
Wanandugu ninataka wa kuanzisha maisha nikiwa na familia yangu nikiwa na mke wangu na pamoja na mtoto wangu

Hivyo ningependa kufahamu ni sehemu gani hapa Dar kuanzisha maisha ambapo ninaweza kupanga vyumba viwili at affordable price na eneo nitakaloishi lisiwe la gharama hivyo naomba kufahamu ni wapi nitaanzia maana mwanamke wangu saivi ana ujauzito hivyo nataka kumtoa kwao nianze kuishi nae
Kwa Mpalange
 
Back
Top Bottom