Ni sehemu gani inakuzwa mananasi, maembe, na machungwa, ambapo mtu anaweza jenga kiwanda cha juice

Ni sehemu gani inakuzwa mananasi, maembe, na machungwa, ambapo mtu anaweza jenga kiwanda cha juice

tajiri tumbo kubwa

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2021
Posts
429
Reaction score
567
Natarajia mko salama wakuu na wanajamii forum. Niko na swali ambalo natarajia hapa ni pahari pazuri pa kupata jibu, sasa nataka kuwekeza kiwanda au viwanda vya kutengeneza juices, toka mananasi.

Maembe na machunga na pia matunda mengine kama passion fruits and mapapai, sasa swali langu ni hili, hapa Tanzania ni sehemu gani naweza pata kilimo cha hizo matunda, yaani kama ni mananasi wapi wilaya gani nanasi zinapatikana kwa wingi, maembe hivyo hivyo,

Machungwa hivyo hivyo, hope munanielewa wakuu na pia mimi naweza pia fanya kilimo cha hayo matunda, yaani nalima na pia nakuwa na wakulima yaani wale tunaita outgrowers, nawapa mbegu na vitu kama hizi wakiwa tayari hayo matunda wananiuzia katika kampuni yangu au kiwanda changu, natanguliza shukrani kwenu.

Asanteni sana, huko nasubiri majibu.
 
Unataka ufungue kiwanda halafu huna bussiness plan! Nakushauri nenda SUA wakuongoze katika hio biashara.

Mkoa wa Pwani una nanasi nyingi, Bagamoyo na Chalinze, machungwa mengi pwani yote na hata maembe na mapapai.

Mkoa wa Tanga una maembe mengi na machungwa mengi sina hakika na nanasi.

Mkoa wa Moro una papai maembe mengi, ndizi, machungwa mengi sina hakika ya nanasi.

Kaweke kiwanda Chalinze uwe centre ya hiyo mikoa hata Dar kuna machungwa mengi.

Nakuongezea Njombe, kuna nanasi nyingi na parachichi nyingi, hata ukitaka kulima papai utafanikiwa.

Mikoa ya kanda ya ziwa na magharibi utapata maembe mengi na mapapai tu.

Mkoa wa mbeya utapata maembe mengi,mapapai na parachichi na ndizi tu.

Passion zipo kwa wingi Njombe.

Unaweza kuwa unasafirisha kupeleka pwani hazina bei.

Nasisitiza nenda SUA kwa wataalamu waliobobea, kiwanda sio kitu kidogo.
 
Kuanzia Chalinze hadi Msata ni sehemu nzuri sana maana ni kama centre. Utapokea matunda toka Moro, Tanga, Bagamoyo, Kibaha, Kisarawe na hata Mkuranga kwa urahisi. Pia maeneo ya jirani yanakubali matunda ya aina mbalimbali.

Hata kiwanda cha Sayona kiko Chalinze (Mboga)
 
Unataka ufungue kiwanda halafu huna bussiness plan! Nakushauri nenda SUA wakuongoze katka hio biashara.

Mkoa wa pwani una nanasi nyingi, bagamoyo na chalinze, machungwa mengi pwani yote na hata maembe na mapapai.

Mkoa wa Tanga una maembe mengi na machungwa mengi sina hakika na nanasi.

Mkoa wa moro una papai maembe mengi, ndizi, machungwa mengi sina hakika ya nanasi.

Kaweke kiwanda Chalinze uwe centre ya hio mikoa hata Dar kuna machungwa mengi.

Nakuongezea Njombe, kuna nanasi nyingi na parachichi nyingi, hata ukitaka kulima papai utafanikiwa.

Mikoa ya kanda ya ziwa na magharibi utapata maembe mengi na mapapai tu.

Mkoa wa mbeya utapata maembe mengi,mapapai na parachichi na ndizi tu.

Passion zipo kwa wingi Njombe.

Unaweza kuwa unasafirisha kupeleka pwani hazina bei.

Nasisitiza nenda SUA kwa wataalamu waliobobea, kiwanda sio kitu kidogo.
Thanks a lot sir, i arleady have a bussiness plan, all what was remaing is to put up such a thread and get more info, i arleady know those areas, i wanted to hear if i can get more info and then i process it, you know data is everything today, thanks again for your info,
 
Kuanzia Chalinze hadi Msata ni sehemu nzuri sana maana ni kama centre.Utapokea matunda toka Moro,Tanga,Bagamoyo, Kibaha,Kisarawe na hata Mkuranga kwa urahisi.Pia maeneo ya jirani yanakubali matunda ya aina mbalimbali.

Hata kiwanda cha Sayona kikoChalinze (Mboga)
Shukrani sana, may God bless you asante sana barikiwa sana
 
Hapa atategemea matunda ya Tanga tu kwa kiasi kikubwa na atapambana na wanaopeleka matunda Kenya
Nataka kuzuia hio ya kupeleka matunda Kenya, kwanini Tanzania tusiwe na viwanda, tupate ajira kwa watu wetu, na hata tu export juices and such mkuu, kazi yetu isiwe tu kuzalisha raw materials au malighafi na taifa zingine kuchukua
 
nataka kuzuia hio ya kupeleka matunda kenya, kwanini tz tusiwe na viwada, tupate ajira kwa watu wetu, na hata tu export juices and such mkuu, kazi yetu isiwe tu kuzalisa raw materials au marigafi na taifa zingine kuchukua

Kwanini uende kwenye competition wakati unaweza kuikwepa? What if competitors akawa stronger than you? Wakati wabongo wanachagua machungwa kwa kuonja kila mti, wakenya wao wanasomba yote. Tanga ni maarufu kwa machungwa na sidhani kama kuna matunda mengine kwa wingi hivyo unaweza India gharama kubwa kusafirisha toka maeneo ya mbali.

Pia Chalinze ardhi bado siyo ghali so unaweza nunua eneo kubwa. Access ya soko ukiwa Chalinze ni nzuri pia.
 
nimeshangaa hakuna mtu hata moja ametaja wilaya ya kasulu, huko kigoma
Soko: Too far to the markert labda kama kiwanda akiweke Kahama.
Lakini kanda ya ziwa na magharibi hakuna matunda mengi kama pwani na nyanda za juu kusini.
Mfano pwani kuna machungwa Kigoma kuna vichungwa vya kukidhi Kigoma tu wakati pwani inauza nchi nzima na nje ya nchi(economic of scale).
Kigoma na Kagera zina parachichi ila haziwexi fikia uzalishaji wa Mbeya, Njombe na iringa hata kwa theluthi tu.

Soko: Pwani ipo karibu na soko kigoma ni mwisho wa reli hivyo ni ghali kiuzalishaji.
Miundombinu: Kigoma bado haijafunguka, haina umeme wa uhakika, maji nk.
Kigoma ina resource sawa ila inakwamishwa na mambo mengi.kama mtu sio mchumi atapeleka kiwanda Kigoma vingivyo hawezi hata kama kuna kila zao.
Watu wa kigoma tutasubiri sana wachu.
 
Back
Top Bottom