Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Pia Kuna Kijiji Cha Msimba na Ng'apa pia Iyovi wilaya ya Kilosa- Morogoro watu wa kule sijui wanaishije maduka hamna Wala shule watoto wanatembe km 30 kufuata shule. Usiku Ni Giza tupu ukisafiri usiku hata usiku wa manane unakuta mtu Teena mwanamke Yuko barabarani na watoto wake wanatembe. Nyumba zao barabara hii wao hapa.
 
Nimekaa mtwara Lind sijakaa ,nimekaa pale ligula mnarani kwa kweli ni fresh Tena karibu na hospital Pako poa sana ningependa huduma zipo halafu watu wachache
Mtwara hakuna vijiji vibaya sana, ni moja ya mikoa ambayo vijiji vyake unakutana na NYUMBA nyingi kabisa, wanakuwa na Soko, maduka yanakuwepo. Kule 90% ya vijiji magari yanafika, nyumba nyingi ni zile za udongo lkn zenye bati na kubwa sio kama vijiji vya kule DODOMA Jmn hadi unajiuliza wanalalaje mule?? Sijui ilikuwaje lkn Mtwara kwenye vijiji wako far better than 80% ya mikoa ya TZ.

Kwangu mimi mikoa ambayo ni ya kijinga zaidi ni DODOMA, KIGOMA, MANYARA, KATAVI, SHINYANGA, MARA na SINGIDA bila kusahau MOROGORO, hiyo mikoa ina vijiji vya ajabu sana sana sana sana.
 
Dodoma ni hatari ,kuna vijiji vinapatikana shortcut (mpwapwa to Iringa road)
Imagine hadi wakiona gari wanakimbia,ilibidi tushuke kwanza tuwauulize maswali ya hapa na pale kuhusu maji,chakula maana Hamna mazao kabisa na vumbi linatimka muda wote ,Vitoto vimebuka hatari unahisi hata wakipiga maji hawatakati,kiswahili pia shida
vijiji vingi hilo limkoa havifai kuishi binadamu.
 
Dodoma ni hatari ,kuna vijiji vinapatikana shortcut (mpwapwa to Iringa road)
Imagine hadi wakiona gari wanakimbia,ilibidi tushuke kwanza tuwauulize maswali ya hapa na pale kuhusu maji,chakula maana Hamna mazao kabisa na vumbi linatimka muda wote ,Vitoto vimebuka hatari unahisi hata wakipiga maji hawatakati,kiswahili pia shida
Et vimebuka[emoji23][emoji23]we itakua mmakonde ww
 
Mwanza miambani wananoishi watia huruma sana japo wao wanaona wamepata viwanja city centre.
Huwa najiuliza walishindwaje kuweka makazi Usagara, Misungwi na Magu badala ya kubanana kwenye mawe kama mijusi ambako kupanda ni shida na inaweza kuchukulia lisaa kwenda sehemu unayoiona kwa mbele tu hapo.View attachment 2378247
Kumbe mpaka lisaa linaweza kukata uko juu vilimani unatembea?
Pikipiki na magari vinafika?
 
Kijiji cha Bugamba Kigoma vijijini mwambao wa ziwa Tanganyika
Kwa mara ya kwanza kufika kijiji cha Bugamba kilichopo mwambao wa Ziwa Tanganyika Kigoma vijijini nilipigwa na mshangao baada ya kushuka kwenye boti kutokea Kibirizi Kigoma ! Pale boti zinapoegesha sikuona nyumba yoyote ! Mwenyeji wangu kaniambia tunaenda nyumbani yaani ananionyesha juu utafikiri tunaenda mwezini ! Kutoka hapo tunapanda huko juu nilitaka kulia maana chini Ziwa Tanganyika juu ndio kijijini, halooo kupanda ilibidi mpaka nishikwe mkono. Kufika huko juu ndoo nakuta kijiji na shule ya msingi ukitizama chini ziwa Tanganyika liko bondeni ! Kwa kweli inatisha kijiji hicho hakuna shamba la maana sehemu kubwa ni milima tu mihogo wanalima kwenye mitelemko ya milima na ukiteleza unaporomokea ziwani na ziwa lina kina kirefu ni hatari. Pale kijijini hakuna baiskeli maana mazingira hayaruhusu ! Shughuli za uchumi pale ni uvuvi. Ukitaka kwenda kijiji cha jirani cha Zashe au Mwamgongo lazima utumie boti kwa mguu haiwezekani.
Toka siku hiyo nikajua sababu ya waha wengi kukimbilia mikoa ya Jirani kama Mwanza, Geita, Tabora na Katavi maana mazingira ya maeneo hayo ni magumu sana. Kweli maeneo hayo ukifika mpaka unajiuliza kwamba hivi hawa watu huku walifuata nini.
 
Uyo mfalme ndio maana alijitenga akaenda mbali ili awafanye watu mazuzu
Kuna kijiji nilifika kutafuta ndizi biashara miaka hiyo.
Aisee ni mbali katikati ya turiani na korogwe njia ya pori kwa pori.hamna magari ni kwenda kwa baskeli tu alafu unachepuka kwenda mlimani huko nikakuta kakijiji aisee vijumba kichekesho,alafu wana mfalme wao yaani chakula wanakula woote familia zoote pale kwa mfalme.
Kila kaya inaleta ilichopika pale.
Nilikula mboga mboga mpk nilikoma.
Siku nikalogwa nikanunua kuku 2 wameniuzia wao wenyewe kaya 1 niliokuwa nakaa nikawapa wapike nikajua ntakula japo nusu aaah wakapeleka kwa mfalme kule tunakokula nikaambulia kibawa,yaani mkulu ana nyofoa kinyama anampa mtu kushoto au kulia kwake kinatumwa mpk kikufikie kila mtu kakishika
Nilikasirika sana.
 
Back
Top Bottom