Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Ndio kule unapenda juu

Waluguru hushuka jumapili kupiga kitimoto pale
Tulienda jumapili moja ni km sherehe hivi
Mkuu Tangeni hapo jirani na Mzumbe University? Hiyo labda itakuwa Bunduki au kule Juu kabisa ya Kijiji kinaitwa Nyandira..
 
Izimbya,, ni sehemu ambayo ipo tofauti na maeneo mengi ya mkoa wa kagera,, pakame, migomba haina afya, ardhi haina rutuba, huduma za kijamii zipo kww manati,, nilistaajabu sana kwa waliouzunguka mkoa huo watakubaliana na mimi
Wewe ni muongo, izimbya ina tatizo la maji tu labda kama ulienda mwaka 2000
 
Mwanga kwenda wapi? Maana kama ni kwenda milimani usangi au ugweno kuna lami mpaka pale Kikweni... Same napo kumekuwa sanaa
Lami ipo mpaka Usangi mbele ya Lomwe Secondary. Magari kama daladala muda wote unashuka mwanga. Bodaboda kibao zinakatisha tu milimani. Umeme, maji ya bomba vipo toka zamani. Shule ni nyingi balaa.
 
Kapanga nimepita majuzi tuu mkuu pamebadilika sana. Mishamo nilifika pia [emoji23] [emoji23]
Tuliendaga kujichukulia ardhi huko, Diwani akaandaa watu tupigane napanga. Noma sana ilikuwa 2013. R.I.P Serengeti, R.I.P Olimaalbert.
 
Uko sahihi kabisa
 
Wewe kilimanjaro una maanisha Moshi, njoo same na mwanga ndiyo utajua hujui. Watu huku wamekauka unaweza kuwapasua kuni na ukapikia maharage yakaiva haraka kuliko stima
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Nimecheka hapa mpaka jamaa amenishangaa ila same ni pamekauka jamani
 
Mkundi,kiegea,makunganya na Majichumvi mkoani Morogoro sijui walifuata kitu gani maji shida, kukame mpaka basi. Duuuuuuuh
 
Duuh..

Hatari sana.
 
Uko mule mule Ila umepuliza
Mkuu izimbya nimeitembea maeneo yote barabara ziko vizuri japo ni changarawe, network kama VODA, tigo na HALOTEL zinasoma 4G isipokuwa maeneo kama kibirizi wanakaaa wanyarwanda, waha na wasukuma. Kuna hospital nzuri pale izimbya pia ni ya KKKT
 
Niliwahi kwenda kijiji kinaitwa Lunenzi, huko wilayani Kilosa. Huko kila kitu kinabebwa kwa kichwa mpaka simenti, nondo, bati etc..
Nimefika huko, hatari sana kwa ustawi wa binadamu.
 
Aaah kmmk walahi..
 
Kweli zama zinabadilika leo hii 825 Kj ni mtabila kasulu kigoma
 
Hii ilikuwq mkoa gn imesound kama home kwetu kbs
Hapo sasa upate na maziwa mgando aisee hatari sana ugali unashuka tu

 

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wanaona kuku ni anasa au hawapendi kula kuku?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wanaona kuku ni anasa au hawapendi kula kuku?
Niliuliza kwanini mnakula mirenda na madagaa kila siku wakati mna ng'ombe na kuku wengi. Nilichojibiwa ni kwamba eti kuku na ng'ombe ni ajili ya kuuzia Watu wa dar wao ni za kulima na kutoa mahali.
Pia nilichogundua jinsi wewe wa mwanza waavyopenda samaki, bukoba wanapenda ndizi na Kaskazini nyama kama chakula chao kikuu Basi na wao Chakula chao kikuu ni mlenda yaani ukimlisha nyama au samaki siku 4 unaweza kumuua mnyaturu😂

Ugali wao ni mgumu mara elfu ya wasukuma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…