Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Ndio kule unapenda juu

Waluguru hushuka jumapili kupiga kitimoto pale
Tulienda jumapili moja ni km sherehe hivi
Mkuu Tangeni hapo jirani na Mzumbe University? Hiyo labda itakuwa Bunduki au kule Juu kabisa ya Kijiji kinaitwa Nyandira..
 
Izimbya,, ni sehemu ambayo ipo tofauti na maeneo mengi ya mkoa wa kagera,, pakame, migomba haina afya, ardhi haina rutuba, huduma za kijamii zipo kww manati,, nilistaajabu sana kwa waliouzunguka mkoa huo watakubaliana na mimi
Wewe ni muongo, izimbya ina tatizo la maji tu labda kama ulienda mwaka 2000
 
Mwanga kwenda wapi? Maana kama ni kwenda milimani usangi au ugweno kuna lami mpaka pale Kikweni... Same napo kumekuwa sanaa
Lami ipo mpaka Usangi mbele ya Lomwe Secondary. Magari kama daladala muda wote unashuka mwanga. Bodaboda kibao zinakatisha tu milimani. Umeme, maji ya bomba vipo toka zamani. Shule ni nyingi balaa.
 
Kapanga nimepita majuzi tuu mkuu pamebadilika sana. Mishamo nilifika pia [emoji23] [emoji23]
Tuliendaga kujichukulia ardhi huko, Diwani akaandaa watu tupigane napanga. Noma sana ilikuwa 2013. R.I.P Serengeti, R.I.P Olimaalbert.
 
Mkuu [emoji23][emoji23][emoji23]
Mimi nina picha kabisa za hivyo vijiji nimefika huko yaani sehemu hata baskeli haifiki. Usafiri ni mitumbwi tu.
Niliwauliza hivi mnajua rais wa sasa hivi ni nani? Wakasema samia nikasema mmejuaje maana huku tv hamna wala network hashiki[emoji23]
Sema yale mazingira ya ziwani mazuri sana kama unataka kufanya retreat ya kujitenga na watu. Ukijani na ziwa + milima milima.
Yaani mtu anaamka asubuhi anaenda kupia mswaki ziwani maana ziwa lipo umbali kama wa mita mia.

Hiyo ya kulima milimani nilishagaa sana maana wakati wa kushukainabidi uwe makini kweli kweli unaweza kuteleza na kuanguka bondeni huko.

Baada ya kwenda hilo eneo niligundua kwanini Wasanii wakipanda kilimanjaro huishia njiai.
Mimi napenda nature, nimetembea mapori mengi humu TZ na kujionea mengi
Uko sahihi kabisa
 
Wewe kilimanjaro una maanisha Moshi, njoo same na mwanga ndiyo utajua hujui. Watu huku wamekauka unaweza kuwapasua kuni na ukapikia maharage yakaiva haraka kuliko stima
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Nimecheka hapa mpaka jamaa amenishangaa ila same ni pamekauka jamani
 
Mkundi,kiegea,makunganya na Majichumvi mkoani Morogoro sijui walifuata kitu gani maji shida, kukame mpaka basi. Duuuuuuuh
 
Vijiji vingi vya wilaya ya Bariadi mkoa wa Simiyu utashangaa wasukuma Sijui walifata nini huko, unakuta kijiji hakina umeme Wala maji. Yaan Maji yao wanachimba mabwawa kipindi cha mvua Maji yanatuama humo basi ng’ombe na binadam wote ndo mnakunywa Maji hayo!! Maji Kama maziwa kuna wachawi huko sijapata ona!! Wanga wananza kuwanga saa moja jioni!! [emoji2][emoji2]
Huko unakuta msukuma ana ng’ombe 50-100 ila anakula ugali na dagaa wa mwanza wale gredi ya mwisho kabisa ambao huwa kwaajili ya vyakula vya Kuku!![emoji2][emoji2] huko ikifika saa 12 jioni tembo kutoka serengeti wanaingia kijiji kula miwa[emoji23][emoji23]
Duuh..

Hatari sana.
 
Uko mule mule Ila umepuliza
Mkuu izimbya nimeitembea maeneo yote barabara ziko vizuri japo ni changarawe, network kama VODA, tigo na HALOTEL zinasoma 4G isipokuwa maeneo kama kibirizi wanakaaa wanyarwanda, waha na wasukuma. Kuna hospital nzuri pale izimbya pia ni ya KKKT
 
Niliwahi kwenda kijiji kinaitwa Lunenzi, huko wilayani Kilosa. Huko kila kitu kinabebwa kwa kichwa mpaka simenti, nondo, bati etc..
Nimefika huko, hatari sana kwa ustawi wa binadamu.
 
Kuna kijiji nilifika kutafuta ndizi biashara miaka hiyo.
Aisee ni mbali katikati ya turiani na korogwe njia ya pori kwa pori.hamna magari ni kwenda kwa baskeli tu alafu unachepuka kwenda mlimani huko nikakuta kakijiji aisee vijumba kichekesho,alafu wana mfalme wao yaani chakula wanakula woote familia zoote pale kwa mfalme.
Kila kaya inaleta ilichopika pale.
Nilikula mboga mboga mpk nilikoma.
Siku nikalogwa nikanunua kuku 2 wameniuzia wao wenyewe kaya 1 niliokuwa nakaa nikawapa wapike nikajua ntakula japo nusu aaah wakapeleka kwa mfalme kule tunakokula nikaambulia kibawa,yaani mkulu ana nyofoa kinyama anampa mtu kushoto au kulia kwake kinatumwa mpk kikufikie kila mtu kakishika
Nilikasirika sana.
Aaah kmmk walahi..
 
Kuna Maeneo yanatisha ndugu, Ziara ya 825 kJ mpwampwa kipindi inarudishwa upya ile kambi maana ilifungwa kwa miaka Mingi sana Kabla ya kuirejesha Eneo la awali ilifanya wengine tutembelee Maeneo mengi ambayo ni tofauti machoni petu kwa upande wa Dodoma ,kuna Kijiji kinaitwa mbuga huko ni baridi si mchezo ndugu na maisha yetu ndio yaleyale.
Kweli zama zinabadilika leo hii 825 Kj ni mtabila kasulu kigoma
 
Hii ilikuwq mkoa gn imesound kama home kwetu kbs
Hapo sasa upate na maziwa mgando aisee hatari sana ugali unashuka tu

Siku moja niko na jamaa yangu tunatafuta mashamba ya kukodi ya alizeti tulikua na mwenyeji anatutembeza mashambani. Mchana tunataka kurudi mwenyeji akatuambia twende kwanza kwake tule ndio tuondoke. Tukaona si mbaya.
Tumefika tukaenda sebuleni Chakula kikaja nikasahau kabisa kama Chakula chao kikuu ni mlenda.
Bwana bwana ulikuja ugali mgumu na mlenda mimi nilikua sijawahi kula mlenda wala ugali wa mtama😅

Nilihangaika mwenye ananiambia mbona hauli au chakula kibaya? Mimi naguna guna tu😂, nilishwindwa kula aisee ilibidi nikaupiga picha hii hapa chini.
Yaani utadhani unakula hina. Watu wanawakiwa na jua huko ndio maana miguu yao imekomaa halafu myembamba kama mianzi imechomekwa kwenye mapaja 🏃🏃View attachment 2379797
 
Watu mna unafiki humu hivi mmeshindwa kutaja vijiji vya Singida kweli???
Watu wa singida vijijini ni watu wa ajabu sana. Imagine mtu ana kuku zaidi ya 50 lakini hachinji hata iweje...Ajabu ni kua hua wanauza kuku ili wapate hela ya kununua mlendawa kusagwa. Yaani huo mlenda unakua kama unakula ugali na hina zile za miti.
Mnyaturu akija kwako usimpikie kuku wala nyama pika mabamia wanapenda makamasi kamasi kwente chakula chao[emoji23][emoji125][emoji125]

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wanaona kuku ni anasa au hawapendi kula kuku?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wanaona kuku ni anasa au hawapendi kula kuku?
Niliuliza kwanini mnakula mirenda na madagaa kila siku wakati mna ng'ombe na kuku wengi. Nilichojibiwa ni kwamba eti kuku na ng'ombe ni ajili ya kuuzia Watu wa dar wao ni za kulima na kutoa mahali.
Pia nilichogundua jinsi wewe wa mwanza waavyopenda samaki, bukoba wanapenda ndizi na Kaskazini nyama kama chakula chao kikuu Basi na wao Chakula chao kikuu ni mlenda yaani ukimlisha nyama au samaki siku 4 unaweza kumuua mnyaturu😂

Ugali wao ni mgumu mara elfu ya wasukuma
 
Back
Top Bottom