Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Mimi ni mwenyehi sana japo kwenye mawe ni mgeni kabisa na sijawahi shawishika kukaa huko juu maana kwa haraka haraka tu ni kwa watu masikini sana kwa hali ya nyumba wanazoishi. Pia mtu mwenye pesa hawezi jenga huko
Nenda Capripoint uone. Kiwanja unauziwa ml 200 na ni juu ya milima na kuna mihekalu ya kufa mtu Mwanza nzima hamna.
 
Pole sana Mwanza ndio ya pili kwa Dar kwa uwingi wa magari hapa Tz.
Naju sana hata mimi napapenda sana na ninapafahamu sana almost kila kona ila kuishi huko milimani mabatinì, igogo, bugando huko nyuma isamilo etc huko kwenye mawe dah siwezi hata bure. Kama mtu una pesa ishi kwenye mawe kama ya capripoint huko kwingine hapana
 
Bora hata mpanda, kuna mahali panaitwa MAJIMOTO aisee huko nilipoenda nilijiuliza qatu wamefuata nini, na wengi wao ni wasukuma kule...Ajabu ni kwamba they are making money ile hatari. Ni matajiri wa kutupwa kutokana na kilimo ufugaji na madini.
Kama wana hela basi ujue ndio walichokifuata huko chaka.
 
Hyo combination ndo yenyewe sasa.hatari hyo.ukipanda haushuki
 
Hapo unakuta hamna vyoo, wanamalizia haja zao makazini/mjini, nyumba za Ibada
 
Watu wanaokaa tukuyu,mwakaleli,katumba kule mbeya, asee wana moyo sana, ni kama watu wanaoishi Dar alafu kipato ni dollar moja.
Tukuyu maisha ni rahisi mno ila pesa ndo hakuna, maeneo kama ushirika, kyimbila, ibolelo, segera, mwakaleli, mpuguso, lusungo kote bila kusahau shamba la chai chivanje
 
Korelo village ~ morogoro vijijini. Nilienda kwenye project huko duh hapana kwa kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…