Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Barabara ya kwenda Kilimanjaro nahisi ni wilaya ya Same Kuna nyumba moja nzuri tu imejengwa kwenye mlima kabisa ipo juu kileleni ipo peke yake ukipita barabarani kwa gari unaiona vzr tu...yule jamaa sijui alifikiria nini kujenga kule juu
[emoji23][emoji23][emoji23] napajua
 
MTWARA ipi?? Mtwara inaizidi mikoa mingi sana Tanzania kwa Maendeleo, Hata vijiji vyake huwezi linganisha karibu na Robo 3 ya mikoa ya Tanzania hii. Unalinganisha Mtwara na mikoa ipi??
Vijiji vya Mtwara kusema kweli sio choka mbaya.. Mambo ya Ushirika yanawasaidia sana na zao la korosho liko vizuri linawapatia kipato na exposure.

Vijiji karibia vyote vya Mtwara vina huduma muhimu za shule, zahanati, maduka, umeme ni maji tu ndio changamoto kwa baadhi ya wilaya kama Tandahimba, Newala na Nanyumbu. Ingawa wenyewe wanachimba visima virefu kuvuna maji ya mvua. Kukuta nyumba nzuri za tofali zimeezekwa msouth kigae au mgongo mpana ni kawaida kabisa.
 
Kasulu Kigoma. Nimeshuka kwenye basi naingia barabarani nakanyaga chini kiatu chote kimezama kwenye vumbi flani laini sana jekundu nikasema dah namna hii mvua zikinyesha panakuwaje si inabidi miguu iwe na 4WD.. Palinichosha mapema sana
 
Kuna Kijiji kinaitwa KWAMASIMBA Kiko wilaya ya Korogwe mjini. Aiseee pale gari zinafika cruiser mkonga tu Tena kwa gear namba moja ikisaidiwa na four wheel LOW.
Umenikumbusha, Korogwe kuna sehemu inaitwa Bungu kama sijakosea. Miaka ya nyuma kidogo 2004 au 2005. Kufika huko kuna kibasi kimoja tu. Na safari nzima kuna vipande vya kutosha mnavyotembea kwa mguu. Halafu kulikua na ushirikina wa kutosha. Kama unaishi kule na wewe si mwenyeji wa kule, siku ukitaka kusafiri kwenda nyumbani kwenu kusalimia au kama unahama hautakiwi kuaga unasepa kimya kimya tu. Yaani raia wastukie upo kwenye gari na mizigo yako. Sasa wewe jifanye ina aga hutoboi Korogwe mjini. Pia mvua ikinyesha nayo ni uchawi tu, kunateleza hata kuku hatembei barabarani na usafiri unakosekana pia
 
Wewe utakua unaongelea Bungu ya Rufiji.
 
Duh!
 
Katikati ya mpanda na kigoma kuna pori wanauza chakula
- Na wanadai kwenda makwao wanatumia zaidi ya masaa 3 kwa mguu; na mtu akitumia gari anachelewa kufika kuliko aliyepita ya mguu. 😂😂😂😂
  • Njia ya Iringa - Dodoma naonaga watu wakitembea barabarani, japo ni tambarare ila lakini vijiji havionekani.
  • Makongorosi - Chunya kule bondeni ziwani kuna kijiji unapita katikati ya kimlima cha miamba kwa miguu. Tuliwafi fika hata wenyeji wakasema, je mmefikaje?, Mmekuja kufanya nini?
 
Kijiji cha kilosa Mpepo wilaya ya malinyi...Kila siku kule ni kupambana na Tembo na Nyati...Masika hakuendeki nilikuwa kule 2020 sijajua saivi pakoje
 
Saivi kuna barabara kabisa inaenda Njombe....Kilimo cha mpunga pako poa tu
 
Weee sasa hivi kuna maji kuna hospital,kuna halmashauri
Kuna mtu alitudanganya ni kama km 6 kutoka ile kona la Kolandoto .Kuna mbuzi wanachoma barabarani kama una roho ya kinyaa huli.Mi nilibonda ,ntarudi tena huko Mhunzee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…