Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Yako wapi ? Kuna watu wanaishi huko nguruwe wanafugwa kama mbuzi huko wanajichunga wenyewe.
Ni wilaya gani kiongozi....ni sikonge, urambo, uyui, nzega, kaliua, igunga au ni wapi huko
 
Uwe unataja Kijiji, kata , wilaya , na mkoa ili watu waelewe unazungumzia eneo gani , sasa kyagata ndio nini na ndio wapi?
Jamaaa ana uelewe mdogo sana anahisi watu wametembea NCHI nzima
 
Kijiji kinaitwa Magwamila kiko Nambendo Wilaya ya Songea ndani ndani uko, wale wayao 95% wote ni watu wa Msumbiji ni mbali kishenzi
Songea ni mbali ajali sasa huko kwingine si ndo kabisa
 
Kijiji kinaitwa Oltukai kipo Kata ya Esilalei wilaya ya Monduli
Kuanzia kimeanzishwa hawajawahi kutumia maji ya bomba na kunafikika kipindi cha kiangazi tuu kwa kupitia mkoa jirani wa Manyara
 
Tabora manispaa kama km 80 kutoka town.
Daaaaah mbona uhakika sema ndo ivooo unaeza letewa singombingo kwamba eneo ni la mradi......kama ni manispa master plan ya mji muhimu.
 
Serikali swala la kufundisha lugha ya taifa wanazembea sana.
 
kibondo kigoma yani, ilikua mwaka 2015 , kwanza kufika uko ni barrier za maana tulikutana nazo barabarani adi nikajiuliza ivi uku ni Tanzania au nchi nyingine.
Kigoma kuna check point nyingi sana, wengine wenye muonekano wa ukanda flan ni mateso sana huko
 
Nilifika mara moja nikiwa na project moja hivi. Jua linaanza kuwa kali saa 3 asubuhi mpaka saa 11 na nusu ukali ule ule yani.
Maji tu kupatikana ni shughuli, hivyo vijiji tu vilivyozunguka wilaya ni kama wapi sijui.
Dar saa 12 asubuhi jua kali kashinda la saa sita mchana don
 
We nae ndio umekosa cha kusema.mpanda watu wanaendesha dualis na harier watu wana hela za madin na ndege ipo dar. Mpanda labda ulifika ya karne ya 12.ila sio mpanda hii mzee
Dualis ni gari ya kuongelea?
 
Tukuyu- masukul niliona panya mkubwa kuliko paka nilipoteza ramani ilikuwa usiku badala ya kwenda kwa babu lwanga nilienda masukulu nilichokiona unforgettable, mpanda-mwese niliona nyoka Kobra kwa macho, kigoma- njia ya maji Kila mtu huko mchawi, tunduru - nilipishana na swala anafukuzwa na simba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…