Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Kuna sehemu nilifika Katesh, Arusha huko, zamani sana. Nilishangaa kukuta wavuta sigara hata magazeti ya kusokotea sigara hawana bali wanatumia mabua ya mahindi. Nilikuwa na gazeti wakafurahi kweli kweli nilipowapa.
Hiyo kijiji kinaitwaje maana kitalangusu,bankero,ata,matangalimo,mitiryangwi huko hakunaga sIgera za dukani wao walisha zoeya kusokota tumbaku kwenye mabuwa ya mahindi halafu wanafuta fegi aisee haya maisha
 
Hiyo kijiji kinaitwaje maana kitalangusu,bankero,ata,matangalimo,mitiryangwi huko hakunaga sIgera za dukani wao walisha zoeya kusokota tumbaku kwenye mabuwa ya mahindi halafu wanafuta fegi aisee haya maisha
Sikumbuki tena jina. Ni zamani sana.
 
Habari za muda huu wanajf.

Nchi yetu ni kubwa na Ina miji na vijiji vingi lakini Kuna baadhi ya maeneo unaweza ukahisi sio sehemu ya nchi yetu mpaka ukajiuliza maswali kuwa Hawa watu waishio hapa walivutiwa na Nini mpaka wakaweka makazi ya kudumu maeneo haya

Mfano, Mimi niliwahi kutembelea Kijiji Cha Baranga kata ya sirorisimba kupitia Kyagata. Nilistajabu na kujiuliza Hawa watu huku wanaishije?

Ukame ndo kwao, maji shida, Hali ya hewa mbovu , jua kali ndo kwao, vurugu Sasa ndo chimbuko lake. Siku moja tulikuwa na mechi ya kirafikina timu ya Kijiji jirani ile tupo kwenye gari tukashangaa tunaanza kurushiwa mawe barabarani.

Kwa kuwa sisi tulikuwa wageni tuliogopa Sana lakini wenyeji wakatuambia msiogope hao wote tutakutana kwenye mnada. Siku nyingine tulikuwa Mnadani Sirorisimba siku hiyo kulikuwa namgogoro wa mpaka wa shamba Kati ya ukoo na uko huku polisi wakiwa na mitutu ya bunduki lakini ilivyo ajabu watu wa kule nilishudia wakibebana na kuhamasishana wabebe mishale waende wakaanzishe vurugu.

Wewe ulipita wapi na ulistaajabu Nini?
Lushoto siyo kubaya ila njia ya kufika huko ndiyo mtihani. Swali lililokuwa likizunguka kichwani ni namna gani mtu wa kwanza kufika kule alifikaje na milima ile.
 
Kuna kijiji kipo katikati ya Kidete wilaya ya Kilosa na Mpwapwa magenge 30 kinaitwa Nana, kwa Mara ya kwanza nilikaa hapo wiki moja bila kuoga, dumu la maji ya mtoni ni buku mnatumia kupikia na kunywa, anayewauzia hayo maji akitoka alfajili kufuata maji na punda anarudi SAA 10 jioni.

Nilipoanza kutafiti maisha yao siku moja Mwenyeji akanipeleka kwa mama mmoja ndio ana club ya pombe za kienyeji ila Mimi nilikwenda kununuwa mihogo asubuhi tuchemshe kunywea chai kambini.

Sasa nikashangaa kila mlevi anayekuja pale amebeba kibegi cha sports mgongoni nikamuuliza mbona hii style siielewi? Akaniambia huku watu hawana pesa ukitaka kunywa pombe unakuja na maindi kwenye kibegi yanapimwa mama muuza anakupa pombe yeye anachukuwa mahindi, aisee Yale maisha ni Bonge la adventure kwangu.

Sehemu zenye madini zina asili ya kutokuwa na maji, madini na maji havikai pamoja, serikali iwahurumie watu hawa kuwapelekea maji maana hata ukichimba visima Mirefu huwezi kupata maji sehemu yenye madini.
 
Bila shaka tulikuwa wote kwenye mkesha wa Mwenge Kijiji cha Ilunde, kule ni noma
Hahaaaa, ni nimetoka huko toka 2014. Huko sio mchezo jamaa nasikia walikuwa wawindaji ndio maana waliishi huko. Niliendaga huko kuwinda Wanyamapori na kuchana mbao za Miminga na Mikora. Operation tokomeza ilinipitia ndio nikakimbia. Maisha haya
 
Kule ni shida tupu kuanzia vianzi taliri mpwapwa kwenda mbele hadi mpwapwa jkt mbele huko kuna shida tupu
Maeneo yale si shida kwa jeshi labda miundombinu ya barabara tu na makazi ya raia ,taliri ndio Inashare Geti na jkt si ndio kila chuo? Vianzi iko direction ipi kwenye ule mji?ni ndani ya eneo la jeshi? Sijaona jina hili Eneo la ramani
 
Kuna kijiji kinaitwa Kasinde kipo mpakani mwa mkoa wa Songwe wilaya ya Mbozi, mpakani mwa Zambia kule.

Kijiji kipo katikati ya mabonde ya mpunga gari zinatoka saa tisa usiku usafiri tu wa pikipiki 40k mvua zikinyesha hakuendeki, halafu ni bondeni hatari unajiuliza watu walifikaje kule hatari sana.
 
Kuna kijiji nilifika kutafuta ndizi biashara miaka hiyo.
Aisee ni mbali katikati ya turiani na korogwe njia ya pori kwa pori.hamna magari ni kwenda kwa baskeli tu alafu unachepuka kwenda mlimani huko nikakuta kakijiji aisee vijumba kichekesho,alafu wana mfalme wao yaani chakula wanakula woote familia zoote pale kwa mfalme.
Kila kaya inaleta ilichopika pale.
Nilikula mboga mboga mpk nilikoma.
Siku nikalogwa nikanunua kuku 2 wameniuzia wao wenyewe kaya 1 niliokuwa nakaa nikawapa wapike nikajua ntakula japo nusu aaah wakapeleka kwa mfalme kule tunakokula nikaambulia kibawa,yaani mkulu ana nyofoa kinyama anampa mtu kushoto au kulia kwake kinatumwa mpk kikufikie kila mtu kakishika
Nilikasirika sana.
 
Tanganyika ndio hatari zaidi
Tanganyika nako sio Mchezo? Kuna vijiji huko Tanganyika tukienda kupora ardhi yaani maarshi yapo ya kumwaga. Tuliendaga kijiji cha Kapanga Tarafa ya Mwese kupora kujigawia ardhi miaka hiyo. Tuliingia kitongoji kimoja, Ng'ombe za wasukuma zikaja na kulizunguka Gari ilikuwa Land cruiser nyeupe na kuanza kuilamba. Tuliendaga Mishamo kwenye kambi za wakimbizi, ukipita Wamama wanakuja kuchukua ule mchanga ambapo tairi la gari limepita eti ni dawa kwa mtoto aliyechelewa kutembea.
 
Back
Top Bottom