Mkuu upo Sahihi unajua wabongo wengi walitawanyika,maeneo kama majengo ambapo ni karibu na Gikomba walikuwepo pale sababu ni karibu na shughuli zao..
Wengine walikuwa wanaishi pale California ni karibu na Majengo pameungana na Eastleigh kuna pilika nyingi za kibiashara pale Eastleigh.
Pale Eastleigh kuna wasomali wengi sana na wengine walitokea kwetu huku Tanzania sasa mpaka ufahamiane nao ndiyo utawajua.
Katikati ya mji wabongo wapo maeneo ya Accra Road kwenye Coast Bus zinapo park Bus za Malindi na Mombasa hapo utawakuta wabongo toka sehem za Tanga.