Ni sehemu ipi NAIROBI wanaishi watanzania wengi?

Nenda soko la mitumba GIKOMBA hapo wakina Mangi wamejaa utazani Rombo
 
Yani unatoka Tanzania unaenda nchi nyingine bado una hamu ya kukutana na hawa magumashi Bongo nyoso?

Bora hata ingekuwa nchi za mbali angalau ningekuelewa, lakini hapo Nairobi unakwenda na Tahmeed tu.

Cha umuhimu uwe na pesa tu basi wala huitaji gozigozi la Wabongo.
 
Mkuu upo Sahihi unajua wabongo wengi walitawanyika,maeneo kama majengo ambapo ni karibu na Gikomba walikuwepo pale sababu ni karibu na shughuli zao..

Wengine walikuwa wanaishi pale California ni karibu na Majengo pameungana na Eastleigh kuna pilika nyingi za kibiashara pale Eastleigh.

Pale Eastleigh kuna wasomali wengi sana na wengine walitokea kwetu huku Tanzania sasa mpaka ufahamiane nao ndiyo utawajua.

Katikati ya mji wabongo wapo maeneo ya Accra Road kwenye Coast Bus zinapo park Bus za Malindi na Mombasa hapo utawakuta wabongo toka sehem za Tanga.
 

Ipo hiyo sehemu pia kuna Makaburi ya Kariakoo maeneo hayo ndipo alipozikwa Bondia Robert Wangira .
Baada ya Waislam kushinda ile kesi ya kuuzika Mwili wake, kesi iliyochukua zaidi ya miezi 8 Maiti ikiwa Mortuary kusubiri maamuzi ya Mahakama.

Siku ya Mazishi yake Kariakoo hapakutosha.
 
Mombasa road, Accra road,jogoo road na west land kidogo pia Karen wapo
 
Ni kweli Gikomba kuna wachaga wengi sana ila wengi wameshalowea huko, ila ukifanikiwa kumpata mtanzania mmoja anaweza kukutambulisha katika vikundi vyao huko utaweza kufahamihana zaidi.
 
Asante mkuu kwa maelezo mazuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…