Nachukia sana
TANESCO kumonopolise soko ,ilitakiwa kuwe na mbadala wa TANESCO ndio maana hawa attend fault kwa wakati ,hawatatui matatizo ya wateja kwa wakati.
Wadau tukomae ili tupate mbadala wa TANESCO ,zaidi ya miaka 60 ya uhuru lakini DSM sehemu kubwa tu hakuna UMEME na huo umeme uliowekwa VIJIJINI ni wananchi ndio wamechanga hela kwa kupittia REA na sio serikali....Tungepata Muwekezaji mwingine apewe kazi ya kusambaza umeme sehemu ambazo haujafika ingekuwa safi sana!!
Tanesco hawaweki huduma sehemu ambayo bado haina makazi ya watu wengi,hapo ndipo kosa linalofanyika ,Tanesco inabidi muweke miundombinu yenu sehemu zote zenye njia kuu au sehemu kwenye mipango miji ni makazi ya watu kwahiyo ikitokea mtu anataka umeme inakuwa rahisi kumuunganishia.