Ni Series ipi uliyoitazama haikufika mwisho na unaona ilikatishwa kimakosa?

Ni Series ipi uliyoitazama haikufika mwisho na unaona ilikatishwa kimakosa?

Sajo

Platinum Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
4,540
Reaction score
8,256
Kila mmoja wetu ana ile series yake (TV Show) ambayo ilimfanya aingie kwenye "addiction" kuifuatilia. Ile ambayo unajikuta unafuta hata ratiba zako za muhimu ili tu upate muda wa kutazama episode nyingine.


Lakini, kuna maumivu ya aina yake pale story inapozidi kunoga, ghafla unakuta kituo cha TV kilichokuwa kinairusha kimeacha kutoa muendelezo! Inakatishwa njiani kwa sababu ambazo mara nyingi huwa hazieleweki au bila hata sababu.

Unabaki na maswali mengi: "Kwanini sasa? Hivi walikosa nini kuisubiri iishe vizuri?" Mbona ngoma ilikuwa na story kali?


Binafsi kuna series mbili ambazo bado zinauma nikizikumbuka:

  1. TYRANT (2014–2016): Hii series ilikuwa moto wa kuotea mbali! Ilikuwa inahusu familia ya rais wa nchi ya kufikirika ya Mashariki ya Kati (Abuddin) iliyokuwa na siasa za ndani, mapinduzi, na migogoro ya kifamilia. Ilipofika mwisho wa Season ya 3, story ilikuwa imefika mahali patamu sana. Ilikuwa na uwezo wa kuwa na mwisho wa kishindo sana, lakini ghafla ikasitishwa, hakukuwa na season 4. Nilimaindi sana na bado siamini kama iliishia pale!
  2. THE BRAVE (2017–2018): Hii ilikuwa inahusu kitengo maalum cha kijeshi cha Marekani kilichokuwa kinafanya operesheni za siri duniani kote. Ilikuwa na action, teknolojia, na suspense ya hatari. Ilianza vizuri sana, lakini ghafla ikakatishwa baada ya Season ya 1 tu. Story ilikuwa bado mbichi, uwanja ulikuwa mpana wa kuendeleza visa vingi zaidi, lakini TV station ikaikatisha njiani.

Ni maumivu ambayo naamini wengi tumewahi kuyapitia.

Je, Ni series gani uliyoifuatilia kwa ukaribu sana, ikaishia njiani kwa kusitishwa, na mpaka leo unaona ilikuwa ni makosa makubwa ya kituo cha TV kuikata? Tiririka hapa chini, hebu tukumbushane machungu ya series zilizotusaliti!
 
The long wait

Vitoto vya elf 2000, mlikuwa mmezaliwa sema hamkuwa na akili
 
Back
Top Bottom