Ni sharti gani ambalo mganga alikupatia na ukashindwa au kukataa kuendelea nalo

Ati mimi na yeye pamoja na viajuza vyenzake sita tukakae uchi kwenye makutano ya barabara kuu hapa Misungwi tena mchana kweupe huku magari yanapita kwa kisingizio kwamba hakuna atakayetuona; na magari yatakuwa yanatupita tu bila kutukanyaga nikasema haloooo!

Msione watu wa huku machimboni wana hela wanasukuma Fortuner mpya zero kilometer mkafikiri mchezo. Watu wamepitia mengi sana japo hawasemi. Ndiyo maana hata kufilisika na kufa kwao ni kugusa tu hasa wakikosea masharti.

Tangu siku hiyo niliamua kujikita kwenye kilimo cha nyanya na dengu. Mambo ya kwenda kukalishana uchi njia panda tena barabara kuu huku malori yakipita full speed tena mchana kweupe hapana aisee! πŸ˜„
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…