Ni sharti gani ambalo mganga alikupatia na ukashindwa au kukataa kuendelea nalo

Yule mzee aliniomba majina yangu na ya mama yangu.

Ilikuwa hivi kuna mjinga alipita na hela zangu nyingi sasa nikiwa na hasira mara pap mitandaoni nikakutana na taarifa zinazomsifia mzee mmoja kuwa ni mganga afu uzuri wake haombi pesa ila anakufanyia kazi ukipata matokeo wewe ndo utajua umlipe kiasi gani, basi bana bila kufikiria mara mbili nikachukua simu nikampigia lakini hakupokea…

Ile jioni akanipigia na kabla sijamwambia kitu akasema kijana mchana nilikuwa na kazi sana haya tuongee sasa ila unaonekana una mazito sana na upo mbali na mimi nilipo nakuomba upange siku uje tuongee na wakubwa(kuna neno aliliongea silikumbuki) nikamwambia kama itawezekana tulimalize kwanza kwa njia ya simu kisha nikiwa naelekea mkoa fulani nitapita hapo mzee wangu. Mzee nikamweleza shida yangu na akasema hiyo kazi ndogo sana. Kabla ya yote akaniomba majina yangu na ya mama yangu. Aiseeee nilitetemeka nikamwambia sawa nakutumia. Baada ya kukata simu niliifuta ile namba na kuanza kujiona jinga kwamba ndo ushirikina unaanzaga hivi na ukizingatia sijawahi hata kuusogelea mlango wa mganga.
 
Kwanini ulikimbia bos?
 
Ati mimi na yeye pamoja na viajuza vyenzake sita tukakae kwenye makutano ya barabara kuu hapa Misungwi tena mchana kweupe huku magari yanapita kwa kisingizio kwamba hakuna atakayetuona; na magari yatakuwa yanatupita tu bila kutukanyaga nikasema haloooo!

Msione watu wa huku machimboni wana hela wanasukuma Fortuner mpya zero kilometer mkafikiri mchezo. Watu wamepitia mengi sana japo hawasemi. Ndiyo maana hata kufilisika na kufa kwao ni kugusa tu hasa wakikosea masharti.

Tangu siku hiyo niliamua kujikita kwenye kilimo cha nyanya na dengu. Mambo ya kwenda kukalishana uchi njia panda tena barabara kuu huku malori yakipita full speed tena mchana kweupe hapana aisee! [emoji1]
Nipe connection ya mganga huyo mm Niko Usagara nimepigika vibaya Sana nikajilipue.
 
Kwanini ulikimbia bos?
Nilijiuliza kwanini atake ajue majina yangu na mama yangu. Je nini sababu nyuma yake: Nilijiuliza nini kitafuata; haya sasa jambo langu lakamilika ila lazima hiki ninachokipanda nitakivuna pia. Je nitavuna nini? Always dark side huwa na mwisho wa uharibifu. That’s all
 
Kuna mshikaji wangu enzi hizo za ujana .Sasa nimemuibukia magetoni namsalimia jamaa kimya tu anaongea kwa ishara tu.Basi ile time inazidi kusogea na jamaa wengine wakawa wanazidi kuongezeka ,kila akisalimiwa kimya anajibu kwa ishara .Akafika jamaa yetu mmoja chamdomo sana akamshikia bango kisawasawa.Jamaa kila akiulizwa akaanza kuwa anatoa jibu moja tu linalofanana kwa kila swali au habari utakayomuuliza.Anasalimiwa mambo yeye anajibu unazingua.Kila anachoambiwa anajibu Unazingua.Badae akajifungia chumbani wana wanae tu,alivyoona kero imekuwa kubwa .Akafunguka mwenyewe kuwa alipewa masherti na mganga asizungumze na mtu yoyote kwa siku mbili.
Hiyo ndio stori yangu ya leo.
Oiii.
 
Nipe connection ya mganga huyo mm Niko Usagara nimepigika vibaya Sana nikajilipue.
Kile kiajuza kilishakata moto mkuu. Kilikuwa kichawi hatari. Kililetwa kule machimboni Geita mwaka 2021 kikaanza kufanya vimbwanga mchana kweupe kwenye duara (mgodi wa mchimbaji mdogo) ya dogo mmoja hivi watu wanakazomea. Kesho yake tu duara ikawaka dogo akapiga zaidi ya bilioni 4 watu wakaanza bibi njoo na kwenye duara yangu kakawaambia mwenye shida anifuate home kijijini Bubale. Unaambiwa mavieite kama yote yalipiga moto hatari kwenda kupanga foleni kijijini. Machimboni aisee kuna mambo ya ajabu sana!
 
Aisee hatsriii
 
Kuna Mzee Mmoja Mlozi Aliyekubuhu huku uswahilini Temeke kila utapomkuta yupo amebeba kibegi mgongoni sasa kwenye kibegi kile habari zinazosemekana ni kwamba kuna maiti ya kichanga ndio nguvu zake na wala hainuki hata tone. Kua Uyaone Ya Dunia
 
Nilidhulumiwa nikaenda anifanyie huyo mwizi anirudishie haki yangu bila shuruti. Akasema huyu dawa yake ni kumtoa roho... Nikashtuka sana. Nikawafikiria watoto wake ... Nikamwambia ngoja nikatafute hiyo pesa nitarudi. Nikatokomea.
 
Back
Top Bottom