Nyafwili
JF-Expert Member
- Nov 27, 2023
- 4,240
- 10,561
Zile siku ambazo tuliishi kuziota kuwa badae yetu, kiasi zimekua mbali na sisi, naam! zile siku tulizoambiana utotoni kuwa tungekuwa hivi na vile.
Siku zilizojengwa kwa dhana na picha ya umaridadi kwamba kabla ya miaka ya muongo wa tatu tutakua tumefika hapa na pale au kumiliki hiki na kile.
Maisha yamejengwa kwenye kila siku moja tunayoishi, ambamo ndani yake kuna mda usioeleweka wa kufurahi, sekunde za uchungu, dakika za kuchoka na saa za kusubiri siku moja ipite ili ije iliyo bora.
Ebu tiririka hapa, ni siku gani hiyo ambayo ilikua bora kabisa katika maisha yako, tag na location.
Da!! kwa upande wangu bado sijapata siku iliyo bora. 🤒🤒