Ni siku ya 17 leo Askofu Josephat Gwajima wa kanisa la GCTC hajaonekana? Wewe unafikiri yuko wapi? Nitakupa Jibu hapa hapa 👇

Kulingana na maono yangu ya rohoni "mganga wake ni ngangari ".
Mganga wake ni Yesu Kristo, Bwana na Mwokozi wa Ulimwengu wote...

Huyu Yesu Kristo ana sifa kuu hizi👇....

1. Ni mganga mkuu wa waganga wote mbinguni na duniani
2. Ni Mungu mkuu wa miungu yote duniani
3. Ni Mfalme wa wafalme wote duniani
4. Ni Bwana wa mabwana wote duniani

#Huyu mganga mkuu na Mungu wa miungu yote duniani na mbinguni akiwa upande wetu, ni nani anaweza kuwa juu yetu...?

Ubarikiwe 🙏🙏🙏
 
Ameshakufa tayari. Watu waovu huwa hawadumu kabisa
 
Kuna watu huwa wanamuona Mungu kama roboti vile. Wanadhani wamemmliki kwa maslahi Yao.
Kuna amri inasema usimjaribu Bwana Mungu wako hata Yesu aligoma kumjaribu Mungu alipoambiwa ajirushe kutoka juu ya jengo .Mungu atamtumia malaika wamdake

Kuvunja vitendo vya kuvunja sheria kwa makusudi kwa kisingizio kuwa Mungu atakutetea ni kumjaribu Mungu
 
Mama inatakiwa afurushwe lakini tusimtegemee Gwajima maana ni muongo muongo
 
Kama hayupo ofisi za ccm atakuwa kwenye maficho yanayojulikana,ila kwa kuwa hawana shida naye wamemuacha hadi picha liishe
 
Polisi kuingilia wameokoa maisha ya raia ambao ilikuwa wafe kama Yale yaliotokea huko Kenya na Uganda kwenye makanisa feki na wachungaji matapeli.
Huyu tapeli Afikishwe mahakani tu.
 
Askofu ameamua kujificha kuogopa mkono wa dola
 
Napinga kuwa Yesu ni mganga mkuu, kwa Wayahudi (tena baadhi) sawa. Mwafrika tafuta mganga wako kulingana na jadi yako.
Pole sana na Mungu akurehemu na kukusamehe kwa kuwa hujui esemalo...

Inakuja siku utakapomhitaji na ndipo utakapom - aknowledge kusema; "...hakika wewe Yesu Kristo ni mganga mkuu..."

Na yeye [huyu mganga mkuu - Yesu Kristo] asema hivi👇👇👇

ISAYA 61:1-2 SUV
"...[1] Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. [2] Kutangaza mwaka wa BWANA uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao;.."​

Na kumbuka hili: Wanadamu HUTIBU lakini Mungu ktk Yesu Kristo yeye HUPONYA

Na kama wewe huamini, yeye siku zote atabaki kuwa wa kuaminiwa kama ilivyoandikwa👇

2 Tim 2:13 SUV
[13] Kama sisi hatuamini, yeye hudumu wa kuaminiwa. Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe.
​

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…