Ni suala la muda tu kabla Ndugai hajakiri au kutamka hadharani kuwa Katiba ya nchi ni mbovu

Ni suala la muda tu kabla Ndugai hajakiri au kutamka hadharani kuwa Katiba ya nchi ni mbovu

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Bnafsi naamini kilichomfanya Ndugai ajiuzulu si mashambulizi(shinikizo) kutoka ndani na nje ya chama chake, bali ni baada ya kugundua Rais hana imani nae huku mhimili anaouongoza Rais ukiwa umejichimbia zaidi. Hivyo, bwana Ndugai akaona hana ubavu wa kupingana nae akaamu kujiuzulu.

Kwahiyo, kutokana na kuonja machungu ya katiba hii, atakuwa na jambo rohoni, na njia pekee ya kutuliza nafasi yake ni siku moja kutoka hadharani na kukiri au kutamka kuwa katiba yetu ni mbovu.

Kumbukeni hakuna kibaya alichosema kilichostahili yeye kujiuzulu zaidi ya kuwa Mhanga wa hii katiba mbovu.


Tunza huu uzi(hii thread) for future reference.
 
🤣🤣🤣
16413170897720.jpg
 
Tena wa namna yake ni mabalozi wazuri katika kuipigani na kupatikana katiba mpya. Tukifanikiwa kuwaingeza wengine watano kama yeye tayari tutakuwa tumefikia lengo la kuipata katiba mpya ya wananchi, tuziweke nguvu pamoja. Mbowe sio gaidi
 
Kweli kabisa na sio yeye tu, wako wengi waliyokuwa wanafaidi maisha kwa kutegemea katiba ya sasa na hasa ubovu/wake. Kwa vile wale waliokuwa wanakula nao sasa wamewageuka lazima nao wateme nyongo.

Ninasubiri kuona ugomvi wa wachawi.
 
Back
Top Bottom