Ni swali tu: Mwenye kujua kuhusu safari ya China aeleze

Ni swali tu: Mwenye kujua kuhusu safari ya China aeleze

KalamuTena

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2018
Posts
13,181
Reaction score
17,187
Huu mwaka ndio huo unakwisha na safari iliyopangwa kufanyika bado.

Ilitegemewa kuwepo safari ya kwenda kuwatembelea marafiki zetu, ndugu zetu, (wasiokuwa mabeberu) tena waliosifiwa kwa kutoweka masharti kama yale ya 'mabeberu' wanapoamua kukupa pesa zao.

Pamoja na sifa hizi tulizowamwagia, hatukukosa pia kuwatapisha tonge walilokuwa wameanza kulimeza.

Tukawanyanyang'a mradi wa Standard Geji, na kama hiyo haikutosha, Bandari ya Bagamoyo nayo hatukutaka marafiki zetu waijenge kwa masharti waliyokuwa wameyapendekeza.

Mtindo huu ndio unaotuonyesha sisi hatubabaishwi na yeyote.

Licha ya yote haya, sisi tumekuwa ndugu wa siku nyingi, na kama vile tunajichanganya wenyewe, CCM yetu na Wacommunist ni pete na kidole. Kwa hiyo wanazidi kuleta mafunzo kwetu tuzidi kukomaa.

Wakatujengea maktaba, na Chuo Kikuu cha Ukombozi Kusini mwa Afrika bila shaka kitajengwa/kinajengwa Kibaha.

Wakati viongozi wengine wa kiafrika wakimiminika kila mwaka, kwenda China kuombeleza,misaada, kupitia mpango wa FOCAC, sisi hatuna shida hiyo.

Kuna siku tutakayopanga sisi wenyewe na marafiki zetu twende huko kwa wakati wetu, kuonyesha kwamba sisi ni tofauti sana na hao wengine.

Uwepo wa safari hii ulishatangazwa, kila mwenye kutaka kujua anajua kuwa safari ilishapangwa. Bila shaka lililokuwa limebaki ni protokali tu, aidha wenyeji waseme wapo tayari kutupokea kwa muda maalum; au sisi wenyewe tuicheleweshe kwa sababu zetu zingine.

Je kati ya hayo mawili ni lipi linalozidi kuchelewesha safari hii, na huku mwaka ndio huu unakwisha?

Tuanze upya kuipanga hiyo safari mwakani huku tukielekea kwenye uchaguzi mkuu?

Safari hii ni muhimu. Ni safari ya kwanza kabisa ya masafa marefu, tena nje ya Afrika.

Hii ni kuwaonyesha marafiki zetu jinsi tunavyothamini urafiki wetu. Heshima iliyoje kupewa wao!
 
saa kumi usiku Mzee unaamkia kutype thread... aiseee kweli tumevurugwa¡!..anyway na Mimi nimeamkia kukomenti dah
 
Niko china mwaka wa saba now , beijing is my second home ... safari ni tamu kinyama nyama
 
Jinsi mambo yanavyokwenda, kila kinachopangwa ujue kinapanguliwa......

Mambo ni mazito hapo Magogoni, hata vitanda havilaliki kwa siku hizi!

Kwani hujamsikia Mzee akilalama, anajuta ni kwanini alienda Dodoma na kubeba fomu ya kugombea!
 
Aende china huku kishamkorofisha DG kipilimba?si atamkuta Kachero mbobezi magogoni tena kajaa tele? ALISIKIKA KOMREDI MMOJA HV ASIERIDHISHWA NA JIWE!!!
 
Hahahha nakumbuka ile simu Mh. Magufuli alipigiwa na Chanceller wa Germany. Au alikuwa Chanceller wa Chato maana alisema ataenda huko Germany ila hadi leo nasiki yupo Chato tu
 
Back
Top Bottom