Ni taasisi ipi ya kifedha ambayo imekuumiza wewe, ndugu yako au Mtanzania mwenzako kwa mikopo yenye riba kubwa?

Ni taasisi ipi ya kifedha ambayo imekuumiza wewe, ndugu yako au Mtanzania mwenzako kwa mikopo yenye riba kubwa?

Enzi na Enzi

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2020
Posts
888
Reaction score
821
Wadau, kupitia gazeti la mwananchi la tarehe 20/12/20 Brg. Gen Mbungo, kamanda wa Takukuru Tanzania ameeleza kuwa, kuna taasisi nyingi zinaumiza wananchi kwa kutoza riba kubwa, ikiwemo kushikilia mali za watu kutokana na mikopo umiza.

Km unauelewa wa taasisi hizo au vikundi hivyo, basi vitaje hapa kwa jina, na mkoa, hii itasaidia TAKUKURU kufatilia taasisi hizo.
 
Ile ya Mama wa Lupaso inajulikana kwa riba kubwa na hamna kitu itafanywa.
 
kwani ulilazimishwa kukopa? hilo ndo tatizo la kutokusoma miongozo ya hizo taasisi alafu unakopa baadae unakuja kulialia
 
Hizi taasisi si zimesajiliwa kisheria? Najiuliza tu kama zinafahamika kwanini Serikali kupitia vyombo vyake haizifuatilii? Inamaana Tz ni shamba la bibi tu.......
 
Tunataka zikopeshe lakini kwa kufuata muongozo wa Bank kuu.
zinatakiwa zisusiwe zisipate wateja uone kama hawatafuata muongozo wa serikali uliowekwa, wananchi kuendelea kuzifuata kwa ajili ya kupata mikopo ndo zinazidi kujimwambafai
 
Hapo ni kweli rudisheni tabasamu kwa wanyonge hasa walimu.
 
zinatakiwa zisusiwe zisipate wateja uone kama hawatafuata muongozo wa serikali uliowekwa, wananchi kuendelea kuzifuata kwa ajili ya kupata mikopo ndo zinazidi kujimwambafai

Hujawahi kupata shida, mkeo anahitaji kufanyiwa upasuaji, au mwanao karudishwa shule, unadhani utakuwa na huo ujasiri wa kususa?? Utakuja ujue baada ya kutoka kwenye shida.
Serikali ndo mlinzi wa wenye nacho na wasio nacho.

Hongera br. Mbungo
Weka jina hapa.
 
naijua shida inavyotesa na kuumiza, hivyo vitaasisi vilivyovingi havijasahiliwa ndo mana vinafanya hivyo.

mwaka juzi nilitaka kukopa somewhere laki 8 ila marejesho yake yanafika hadi 1.62 milion nkatoka nduki.

bora ukope vikoba kule hakuna shida
 
Back
Top Bottom