Ni takwimu za kutisha sana katika Mahusiano/Ndoa. Kuna jambo tunapaswa kujifunza tupende tusipende ama sivyo tutaangamia

Mbona 500 ni chache Sana ukilinganisha na ndoa zinazofungwa.
Ishu ya ndoa ni maturity ya wanandoa na sio usomi. Kuwa na vyeti hakumaanishi wewe ni maturity.
 
Athari ya talaka kwa watoto ni kutokuwa na upendo kwenu wazazi hata akishakuwa Mkubwa hawezi kuwa karibu nanyi sababu ya ile laana ya kuachana.
 
Ukweli mchungu!!
 
Vp kwa watu wa pwani ambao kwao kufunga ndoa wakiwa na umri mdog wa kuanzia miaka 20 ni jambo la kawaida nao tunawahukumu vipi?
 
Huo ulikuwa unamfanya mwanamke ajione yeye yupo duniani kwa ajili ya kuolewa. Hata akiwa na elimu ama nafasi kubwa na mchango katika jamii, bila kuolewa anajiona hana thamani. Je, wewe unadhani ni sawa?
Ni sawa kabisa wala si utani
 
Wanawake wenye sifa za kuolewa ni wachache na wanaume wenye sifa za kuoa ni wachache pia. Ndoa Ina kanuni na misingi yake KILA mwanandoa anao wajibu wake apaswao kuutimiza.
 
Makahaba na michepuko utumia madhaifu ya wake waliolewa kutotimiza wajibu wao kwa kuzitumia mbinu hizo kuwaiba wanaume za watu. Wanawake wengi seminar ya ndoa ikiisha na yote waliojifunza uyaacha pale pale kwenye seminar, so michepuko na makahaba utumia Yale mafundisho ya ndoa kuiba na kuteka wanaume za watu.
Cha ajabu hata hao makahaba na michepuko nao wakiolewa na wanaume waliowapora nao urudia makosa Yale Yale wafanyayo wanawake wa kwenye ndoa.
Muhimu ni kujifunza kuishi nao.
 
Umasikini ndio unaowasukuma wanawake wengi wakiwemo hao wasomi kuingia kwenye ndoa, so umasikini wao ukiisha au wakimudu kujitegemea ile nguvu ya msukumo utoweka, tofauti na wanawake waliosukumwa na nguvu ya upendo kuingia kwenye ndoa.
 
Naunga mkonyo hoja.
Jando na Unyago ni elimu nzuri sana. Inachotakiwa ni kuiboresha tu kuendana na nyakati tulizo nazo sasa, bila hii hizi kesi za familia kuvunjika zitaendelea sana hadi akili itapotukaa sawa.
 
Umasikini ndio unaowasukuma wanawake wengi wakiwemo hao wasomi kuingia kwenye ndoa, so umasikini wao ukiisha au wakimudu kujitegemea ile nguvu ya msukumo utoweka, tofauti na wanawake waliosukumwa na nguvu ya upendo kuingia kwenye ndoa.
Uzi ufungwe, hii ndio sababu ya wanawake wengi kuolewa sikuhizi. Shida zikiisha mwanamke haoni sababu ya kuendelea kumpenda na kumtii mumewe.
 
ukweli mtupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…