Ni Tanzania pekee baada ya ligi kwisha kamati inakaa kuchagua mfungaji Bora, kwanini kanuni isiwe wazi mwanzoni mwa msimu?

Walisahau kujua km kuna magoli ya assist, penalties, dakika chache za kucheza pia mchezaji km alifunga magoli akiwa timu nyingine je ataitwa mchezaji bora wa timu ama wa ligi
 
Wondering
 
Hivi ni nani amesema kwamba kamati itakaa kuamua nani mfungaji bora?

Lakini pia kuna mfungaji magoli mengi(top scorer) na tuzo ya mfungaji(Golden boot)

Kuna mashindano hayatoi tuzo kwa mfungaji magoli mengi ila inawatambua tu kama top scorer
Hapa hata wakilingana watatajwa wote kama top scorers
Kwenye tuzo(golden boot) kama kanuni za mashindano zinataka mmoja tu basi kanuni huwa zinawekwa wazi ili kuleta mzania sawa kiushindani
Kanuni zaweza kuwa
Assist
Penalty
Idadi ya mechi nk

Hizi kanuni zinapaswa kuwa wazi kabisa kama ambavyo unaweza kupata za FIFA Wc au EPL au La Liga nk

Lakini hapa naona reference pekee inayotolewa ni kipande cha quote ya afisa habari wa TFF mwaka 2021/22 alipotamka wakati mayele na mpole wanakimbizana magoli
Inabwezekana zikawa ni zilezile au zimebadilishwa
Hatujui kwasababu TFF hawajaweka wazi kanuni zote za mashindano wazi

Kwa dunia ya sasa ni aibu kwa ligi kwisha na hakuna anayejua kwa hakika kanuni zinasemaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…