Ni Tanzania pekee baada ya ligi kwisha kamati inakaa kuchagua mfungaji Bora, kwanini kanuni isiwe wazi mwanzoni mwa msimu?

Ni Tanzania pekee baada ya ligi kwisha kamati inakaa kuchagua mfungaji Bora, kwanini kanuni isiwe wazi mwanzoni mwa msimu?

Yaani sijui nani katuroga!
Basi kama kulikua hakuna hizo kanuni kwanini msikae juzi baada ya mechi ya Simba Maana tayari kulikuwa na dalili ya Saido kulingana na Mayele!
Kwanini yaani!

Eti ooh,
Kamati ndio itakuwa!
Kamati my foot!

Suala la mfungaji Bora wala halihitaji kamati ni kanuni tu, itategemea zimepangwa kwa mtiririko upi,

Kwamfano FIFA, kombe la Dunia wao waliweka (kama magoli yamelingana) basi watatumia
1. Assist
2. Dakika chache za kucheza.
3. Magoli ya Penalties

Sasa hapa kwetu HAKUNA AJUAE!
Sawa ngoja kamati imchague Mayele au Saido
Walisahau kujua km kuna magoli ya assist, penalties, dakika chache za kucheza pia mchezaji km alifunga magoli akiwa timu nyingine je ataitwa mchezaji bora wa timu ama wa ligi
 
Iko hivi, kwenye zile kanuni kuu za Ligi huwa haiwekwi, hizi huwa ni kanuni ndogo za michuano. Nenda hata CAF hakuna sehemu wameweka utaratibu wa Top Score but wanajua kuna mfungaji bora nk. Kuna kanuni kuu na ndogo, kanuni ndogo zipo TFF na kanuni kuu za Ligi huwa zinakuwa Published.

Watu mnachanganya TOP SCORE vs GOLDEN BOOT.

Wote mnaweza kuwa Top Score lkn haiwezekani wote mpate Golden Boot kwenye michuano mingi.

Kwa Bongo Top Scores ni MAYELE 17 [emoji460]️
SAIDO 17 [emoji460]️

Ila Golden Boot atapata MAYELE kwa kuwa ana magoli machache ya penati.
Wondering
 
Hivi ni nani amesema kwamba kamati itakaa kuamua nani mfungaji bora?

Lakini pia kuna mfungaji magoli mengi(top scorer) na tuzo ya mfungaji(Golden boot)

Kuna mashindano hayatoi tuzo kwa mfungaji magoli mengi ila inawatambua tu kama top scorer
Hapa hata wakilingana watatajwa wote kama top scorers
Kwenye tuzo(golden boot) kama kanuni za mashindano zinataka mmoja tu basi kanuni huwa zinawekwa wazi ili kuleta mzania sawa kiushindani
Kanuni zaweza kuwa
Assist
Penalty
Idadi ya mechi nk

Hizi kanuni zinapaswa kuwa wazi kabisa kama ambavyo unaweza kupata za FIFA Wc au EPL au La Liga nk

Lakini hapa naona reference pekee inayotolewa ni kipande cha quote ya afisa habari wa TFF mwaka 2021/22 alipotamka wakati mayele na mpole wanakimbizana magoli
Inabwezekana zikawa ni zilezile au zimebadilishwa
Hatujui kwasababu TFF hawajaweka wazi kanuni zote za mashindano wazi

Kwa dunia ya sasa ni aibu kwa ligi kwisha na hakuna anayejua kwa hakika kanuni zinasemaje?
 
Back
Top Bottom