Ni Tanzania tena Kimataifa! Shirika la Ndege la Kimataifa la Uswisi lazindua safari zake kuja Tanzania

Ni Tanzania tena Kimataifa! Shirika la Ndege la Kimataifa la Uswisi lazindua safari zake kuja Tanzania

Hii ni moja ya sababu iliyonifanya niipende Serikali ya Awamu ya Sita! Hawana kelele sana wala propaganda ni vitendo tu na matokeo yanaonekana.

Baada ya Serikali iliyopita kudharau Sera ya Mambo ya nje jambo lililopelekea Tanzania kutofaidika na Sera Bora ya Mambo ya Nje, Sasa Mabadiliko ya Sera ya Mambo ya Nje tunaanza kuona yanaanza kuzaa matunda.

Kufuata miongozo ya kimataifa juu ya Corona na kuzingatia upya mahusiano bora na mataifa mengine kunaanza tena kuifaidisha Tanzania Kiuchumi.

Leo Shirika la Ndege la Kimataifa la Uswisi limeanzisha Safari zake kuja Tanzania! Na kwa Leo tu wameshusha watalii 270 Uwanja wa ndege wa kia

Kwa msiojua kila Mtalii anapotua tu hapa Tanzania analipia dola 100 kama gharama ya visa. Hapo hujalala hotelini ambapo TRA wanaingiza Tourist tax, Hapo hajaenda mbugani ambapo analipia pia kama dola 100 kwa kuingia tu mbugani. Fedha zote hizi zinaenda kumuhudumia Mtanzania Kwa kumpatia Maendeleo.

Kusema kweli sina budi kumpenda Mama Samia! Ndo mana thamani ya Shilingi ya Tanzania inazidi kuimarika dhidi ya dola ya Marekani. Hongera Kwa Mabadiliko ya Kisera yanayozidi kulinufaisha TaifaView attachment 1969580View attachment 1969581View attachment 1969582
👏👏👏 lakini walisitisha lini safari zao za Tanzania au zilikuwa sababu za Corona kwa sababu hili janga limetesa sana mashirika ya ndege na biashara ya utalii kwa ujumla.
 
Kwani hii ndio picha ya kwanza ya ndege za watalii kutua KIA tangu awamu hii ingie madarakani? Wakati wa awamu ya Hayati JPM picha hizi zilikuwa nyingi tena kipindi corona imepamba moto huko duniani.
 
👏👏👏 lakini walisitisha lini safari zao za Tanzania au zilikuwa sababu za Corona kwa sababu hili janga limetesa sana mashirika ya ndege na biashara ya utalii kwa ujumla.
Sina taarifa kamili! Inaonekana ndo wameanza baada ya kipindi kirefu au hawakuwa wanakuja kabisa!

Sidhani kama walisitisha kipindi cha corona
 
Kwani hii ndio picha ya kwanza ya ndege za watalii kutua KIA tangu awamu hii ingie madarakani? Wakati wa awamu ya Hayati JPM picha hizi zilikuwa nyingi tena kipindi corona imepamba moto huko duniani.
Jaribu kutofautisha picha za kupokea watalii na picha za shirika la ndege kuanzisha Safari za kuja Tanzania
 
Vitu vingine kama huvijui nyamaza
Ongea vichache tu unavyovijua
 
Hana maneno mengi kama yule bwana aliyenifanyaga niichukie ccm ila kwa mwendo huu nasema hivi "NIMEREJEA KUNDINI"🤗
Wakati wa Magu mbona ndege zilikuwa nyingi za kitalii........
ama mnajisahaulisha kijinga!!?
 
Kwani hii ndio picha ya kwanza ya ndege za watalii kutua KIA tangu awamu hii ingie madarakani? Wakati wa awamu ya Hayati JPM picha hizi zilikuwa nyingi tena kipindi corona imepamba moto huko duniani.
Achana na washamba hao......
hawajielewi kama kuku wa kizungu
 
Fisadi lililozuiwa mirija ya ufisadi linachekelea, kwa taarifa yako hata awamu ya 6 huwezi kupiga
Fisadi tenaaa??? Mm ata salary ya serikali siijui ilivo ndugu😂😂😂😂
 
Fisadi lililozuiwa mirija ya ufisadi linachekelea, kwa taarifa yako hata awamu ya 6 huwezi kupiga
Fisadi tenaaa??? Mm ata salary ya serikali siijui ilivo ndugu😂😂😂😂
Wakati wa Magu mbona ndege zilikuwa nyingi za kitalii........
ama mnajisahaulisha kijinga!!?
Tatz kwangu siyo ndege, tatz lilikuwa utawala wake tu wa mabavu basi
 
Back
Top Bottom