Watanzania wamekereka kweli kweli na wanataka mabadiliko.
Wanataka katiba mpya. Wanataka wabadhirifu wawajibishwe. Wanataka utawala bora, hawataki uwakilishi wa walamba asali au wa wahuni nk.
Yote mema kabisa. Tatizo kubwa ni kuwa wanayataka mema hayo wakiwa unorganized. Matokeo yake wamekuwa ni kama genge la wenye kuyataka mema hayo kwa maneno si kwa vitendo.
"Wamekuwa genge la watu ambao wangependa yule au wale wafanye vitendo lakini si wao."
Ifahamike kuwa mabadiliko hayataletwa na walamba asali, wahuni au wale vijana wa hovyo. Kwa huruma zao au kuwalilia hali.
Vile vile tufike mahali tuambiane ukweli. Wenye maneno matupu au maoni, ni heri wakakaa nayo tu. Hayahitajiki!
Tumeyaona kote kwingine Kenya, Zanzibar, SA nk. Vinahitajija vitendo? Wako wapi kina Raila, Maalim Seif, Tutu, Mahlangu, Biko, Mandela au Malema?
Siyo siri tena. Kwa hapa tulipo hatunao viongozi wa kutuongoza kwenye tunayoyataka. Hapa ndipo pa kuanzia:
"Tupange safu za viongozi wetu kulingana na matokeo tunayotaka."
Tupite kwenye primaries tusikie mikakati ya kila mmoja anayetaka uongozi. Asiyefaa akae pembeni au tumweke pembeni.
Hizi nyimbo za kuwalaumu wafuasi wakati wanaofisha jitihada hizi wanajulikana ni muda sasa zikakoma.
Uongozi usiwe fursa. Uongozi ni mzigo. Uongozi una risks. Uongozi ni kuwajibika. Uongozi si lele mama.
"Joto likikuzidi unawaachia wengine."
Luka 18: 18-27 -- alipoambiwa kuuza kila kitu awape maskini ....
"Mitu ya Fursa."