Ingawa sijui kipato chako kikoje ila kwa amount uliyoloose kibongo bongo sio ndogo! Lazima itakuondolea confidence kimtindo.
Hivyo umewaza vizuri sana kutafuta kampani ya kutrade nao kwa maana ya ku gain confidence
Ushauri wangu, kati ya hao uliowataja juu kama umejiridhisha vya kutosha ningekushauri u trade na Forex Money industry ambao nadhani wako chini ya Fransisco magnetic. Huyu ni trader wa muda mrefu bila kujalisha yaliyomkuta hapo katikati lakini pia sio aina ya watu wa majigambo (wakati mwingine majigambo yanapofusha tu)
Wengine ninaowafahamu ni KasheboFx, Market Switch, Afriforex (hawa sasa hivi wana program ambayo haina kutozana hela ila tu uwe na account avatrade kwa link yao), na Mac empire (July boy mwenyewe anajiita)
Kashebo ni rahisi zaidi kumfuatilia maana kila weekend anafanya analysis free utube na kwenye telegram group lake pia anafanya account management
NB: Sijawahi kuwa kwenye VIP group zao wote hao ila kazi zao zinaonekana na wanaotrade nao wanawasema vizuri na sijawahi kusikia skendo yoyote kuwahusu tangu nianze kuwafuatilia (2017)!
Lakini pia sio lazima utafute hizo timu za kulipia! Kuna watu kibao wanatrade kama timu bila kutozana hela yoyote! Yaani mnafanya analysis kwa pamoja, mnabishana, na kisha mnaamua entry kwa pamoja. Hapa unaweza kutafuta watu unaofahamu uwezo wao mkaji organize kwa pamoja
Ni hayo tu! Changamoto unazopitia ni za kawaida sana.