Ni timu gani kati hizi tano nijiunge nayo kwa ajili ya `Signal Subscription’ wakati na mimi najifua mdogo mdogo

Ni timu gani kati hizi tano nijiunge nayo kwa ajili ya `Signal Subscription’ wakati na mimi najifua mdogo mdogo

Kapena

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2017
Posts
376
Reaction score
507
Nimeanza rasmi kusoma kwa undani issues za Stock Market (Forex, Commodities, Indices, Future nakadhalika)

Nimepiga hesabu naona nahitaji at least miezi mitatu hadi nianze ku invest serious kwenye stock market.

Wakati najifua, nimefikiria bora nijiunge kwenye timu inayotoa Signal subscription ama Account management.

Kwa nini?

Kupitia timu hiyo nitakua najifunza practically strategies zao wanazotumia. Hivo theory na practical vinaenda pamoja.

Pia kama service ikiwa reliable nitakua nakuza account mdogo mdogo.

Sasa hapa bongo kuna timu kama tano popular zinatoa signals and account management.

Nahitaji mliojiunga mniambie kati ya hawa washkaji timu gani ipo reliable nijiunge nao wakati najifua mdogo mdogo.

255_Millionaires_Fx
Washkaji kila jmosi lazima wapost profit vs loss za week nzima.

Fx_Money_Industry.
Huyu mshikaji Magnetics naona yuko vizuri. Sijui ashaanza kuwalipa wadai wake.

Uptrend_Inc
Timu ya Udhaifa na Ontario wake. Sema sionagi wakipost sana mrejesho wa kila week.

Forex_Elites_Academy
Hawa washkaji kina Kapinga naona wako vizuri pia.

Elikana_Fx
Huyu mshikaji yuko vizuri pia, sema jamaa anacharge $100 kwa mwezi duh!!

Kuna waliojiunga mojawapo ya hizo signal groups anipe feedback timu gan nzuri ya kujiunga nayo. Nikuze account pia nijifunze strategy zao.
 
Nakushauri sana usome forex bila mihemko..achana na kutumia singnal za watu wanaotamba mitandaoni.

Mimi nimechoma sana account Kwa signal za watu lakini baada ya kuacha signal za watu na kujiamini ukweli nimeona matokeo ya forex na ninajipanga kuwekeza nguvu zaidi na muda.

Iko hivi katika signal tatu wanazotoa kuwa zimekubali naamini signal tano zimekufa. Ni bora uwe na principal yako personal ambayo itaendana na mtaji wako na uelewa wako
Kumbuka MTU anayekupa signal haujui mtaji wake ukoje.mfano wewe labda unamataji wa dola 50 lakini anayekupa signal anamtaji wa dola 1000, wakati yeye anauwezo wa kuhold lose wewe tayari umechoma account halafu baada ya mda anakuja kupost faida wakati wewe umeshatoka sokoni na umeenda Kwa templer kwenye kale kamkoni kalikoandikwa deposit.

Na Mimi nilishauriwa haya niliyoandika lakini sikuwasikia na nilichopata nakijua mwenyewe.
Mfano hai wangu.kuna siku nilitumia signal za jamaa Fulani ni mzuri sana kufundisha YouTube na video zake zimenisaidia sana..siku hivyo niliporomoka hadi dola 4 balance kabla sijaunguza nikatoka sokoni haraka.halafu nikaanza kutumia uwezo wangu na uelewa wangu..huwezi amini ndani ya masaa matatu nilikuwa nimetengeneza dola 20 na zaidi bila kutumia signal za mtu
 
Soma tu mkuu ila hizo profit wanazoonyesha hazina ukweli Kwa asilimia kubwa invest kwenye elimu tu

Ushauri lipia sana elimu kuliko signal
 
Anayetaka kujifunza forex PM kwa maelezo zaidi ada Tzs 1,000,000/- Fixed
 
Ushauri wangu kwako ili ufanikiwe inabidi ujijue ww ni trader wa aina gani (scalper, intraday, au swing trader).

Kisha ujijue kama unapenda kutumia naked chart au indicators kuchambua soko.

Baada ya kupata majibu ya hayo maswali ndo utafute mentor wa kuendana na mahitaji yako.
 
Ningekufundisha ila muda sina ungelipa ya bando tu kwa indro na partial basic ila advanced ungelipa 30$
 
Ningekufundisha ila muda sina ungelipa ya bando tu kwa indro na partial basic ila advanced ungelipa 30$

Mimi sio beginner kivile jombaa.
Two years ago, nilishawahi kutrade kwa miezi kadhaa kabla sijaacha baada ya kuwa nachoma account tu.

Nilienda kupiga kwanza shule. Sasa shule imeisha. Ndio nataka nirudi tena.

Habari za fundamental analysis, risk management, candlestick charts, SMA, EMA, MACD indicators vyote nina idea navyo.

Nilishaijunga huduma ya Account management kwa washkaji wanajiita CMC kama unawajua. CEO wao ni Gammy.

Nikaishia kuchoma account ya $1500.

Kuna mshkaji anaitwa Gasper. Alishanichomea $2000 hivi live naona.

ina maana ndo kusema hapa Bongo hakuna kabisa reliable account manager mkuu?

Mimi sasa hivi nachopigania ni kupata reliable trading strategy. Nitafurahi sana.

Kifupi hata nikisikia kuna training ya Forex basi iwe kwenye Advanced Stage.

Nahangaika sana. Lakin nachangaa kuna watu naona wamefanikiwa (kupitia accounts zao za Insta na WhatsApp)

Sijui inakuaje hii.
 
Mkuu kwanini hizo hela kama kweli unahitaji mentor na signal usijiunge na yule jamaa wa baby pips?

Forex ni nzuri kama una trade mwenyewe bila kutegemea signal za mtu@Kapena,
 
Mkuu kwanini hizo hela kama kweli unahitaji mentor na signal usijiunge na yule jamaa wa baby pips?

Forex ni nzuri kama una trade mwenyewe bila kutegemea signal za mtu

Anaitwa nani, nampataje, najiungaje.
Anatumia account yani insta etc.
 
Kama hautajali kuna jamaa anafundisha BTMM mtafute telegram kama utamuelewa ni sawa...
Anaitwa Jeff ila jina la telegram ni lingine..
Na kuna mwingine anafundisha Kwa dola 40 huku anatoa na signal ila Jeff yeye Kwa sasa anacharge dola 79 Kwa mwezi ila ni mtalam Wa btmm sana hope hautajuta
 
Akili kichwani mkuu.. inawezekanaje mtu anapost mafaida ya maelfu ya dola kila siku bado akomae na wanafunzi wampe dola mia kwa mwezi? Don't be a sheep bro ...@Kapena,
 
Akili kichwani mkuu.. inawezekanaje mtu anapost mafaida ya maelfu ya dola kila siku bado akomae na wanafunzi wampe dola mia kwa mwezi? Don't be a sheep bro ...

Assume una group lako WhatsApp unatoa signal service. Una charge $100 kwa mwezi kwa kila member. Group lina members 50.

Huoni kuwa kila mwezi utakua na uhakika wa kuingiz extra $5000 kama fee ya kutoa service yako.

Hata kama mtu anaingiza mpunga mrefu, haimzuii kutafuta vyanzo vya ziada vya income.
 
Kapena,
namaanisha kuwa kama uko level ya kumiliki ndinga kama Maserati utakomaa no tudola mia?anyway to each his own lilikuwa angalizo tu mkuu pesa ni yako spend unavyoona inafaa
 
namaanisha kuwa kama uko level ya kumiliki ndinga kama Maserati utakomaa no tudola mia?anyway to each his own lilikuwa angalizo tu mkuu pesa ni yako spend unavyoona inafaa

Poa. Sema nini, unaonekana kama mshamba hivi. Hujui principle za cash flow.
Nyinyi ndio wale ukiona 500 barabaran huokoti kisa una 10,000 mfukoni.
Acha ushamba. Elimika. Fatilia principle za active and passive income ujanjaruke.
 
asante sana chief....
 
Mimi sio beginner kivile jombaa.
Two years ago, nilishawahi kutrade kwa miezi kadhaa kabla sijaacha baada ya kuwa nachoma account tu.

Nilienda kupiga kwanza shule. Sasa shule imeisha. Ndio nataka nirudi tena.

Habari za fundamental analysis, risk management, candlestick charts, SMA, EMA, MACD indicators vyote nina idea navyo.

Nilishaijunga huduma ya Account management kwa washkaji wanajiita CMC kama unawajua. CEO wao ni Gammy.

Nikaishia kuchoma account ya $1500.

Kuna mshkaji anaitwa Gasper. Alishanichomea $2000 hivi live naona.

ina maana ndo kusema hapa Bongo hakuna kabisa reliable account manager mkuu?

Mimi sasa hivi nachopigania ni kupata reliable trading strategy. Nitafurahi sana.

Kifupi hata nikisikia kuna training ya Forex basi iwe kwenye Advanced Stage.

Nahangaika sana. Lakin nachangaa kuna watu naona wamefanikiwa (kupitia accounts zao za Insta na WhatsApp)

Sijui inakuaje hii.
Ingawa sijui kipato chako kikoje ila kwa amount uliyoloose kibongo bongo sio ndogo! Lazima itakuondolea confidence kimtindo.

Hivyo umewaza vizuri sana kutafuta kampani ya kutrade nao kwa maana ya ku gain confidence

Ushauri wangu, kati ya hao uliowataja juu kama umejiridhisha vya kutosha ningekushauri u trade na Forex Money industry ambao nadhani wako chini ya Fransisco magnetic. Huyu ni trader wa muda mrefu bila kujalisha yaliyomkuta hapo katikati lakini pia sio aina ya watu wa majigambo (wakati mwingine majigambo yanapofusha tu)

Wengine ninaowafahamu ni KasheboFx, Market Switch, Afriforex (hawa sasa hivi wana program ambayo haina kutozana hela ila tu uwe na account avatrade kwa link yao), na Mac empire (July boy mwenyewe anajiita)

Kashebo ni rahisi zaidi kumfuatilia maana kila weekend anafanya analysis free utube na kwenye telegram group lake pia anafanya account management

NB: Sijawahi kuwa kwenye VIP group zao wote hao ila kazi zao zinaonekana na wanaotrade nao wanawasema vizuri na sijawahi kusikia skendo yoyote kuwahusu tangu nianze kuwafuatilia (2017)!

Lakini pia sio lazima utafute hizo timu za kulipia! Kuna watu kibao wanatrade kama timu bila kutozana hela yoyote! Yaani mnafanya analysis kwa pamoja, mnabishana, na kisha mnaamua entry kwa pamoja. Hapa unaweza kutafuta watu unaofahamu uwezo wao mkaji organize kwa pamoja

Ni hayo tu! Changamoto unazopitia ni za kawaida sana.
 
Back
Top Bottom