Mkongwe Mzoefu
JF-Expert Member
- Aug 10, 2018
- 861
- 2,515
Mtu katumika maisha yake ya ujana kwa taifa, wengine wamepigana hadi vita ndani na nje ya nchi kwa uaminifu mkubwa lakini ndani ya miaka 20 hakumbukwi na hapo kazidi kuwa kikongwe lakini hakuna kiongozi au wabunge (ukiacha Esta Bulaya, Mungu ampe maisha marefu) anaye jali.
Ni tokea Kikwete apandishe pension ya wastaafu wa Hazina toka 25,000 hadi Laki moja miaka 20 iliyopita hajatokea mwingine kuwaza hawa wazee lakini angalia mishahara yao na marupurupu yao leo na miaka 20 iliyopita!
Pengine hata hayo mawazo ya wazee kumuwazia Kikwete arudi madarakani kama Trump yanaweza kuwa sawa, kwanza kiumri Trump ni mzee kuliko Kikwete.
Au mnasemaje kuhusu mawazo haya ya wazee?
Soma makala hii ya Mwananchi utaelewa vizuri
www.mwananchi.co.tz

Siku mstaafu alipoongezwa pensheni kwa mara ya mwisho
Kama utani, wastaafu wetu wa kima cha chini wanafikisha miaka 20 sasa tangu yule mwana mwema wa Msoga alipoamua kuwapa nyongeza ya pensheni yao ya Sh50,000 kwa mwezi, kuwa Sh100,000.