Ni tokea Kikwete apandishe pension ya wastaafu wa Hazina toka 25,000 hadi Laki moja miaka 20 iliyopita hajatokea tena

Ni tokea Kikwete apandishe pension ya wastaafu wa Hazina toka 25,000 hadi Laki moja miaka 20 iliyopita hajatokea tena

Hawa ndio watoto walioliachia taifa! "unazan" unadhani litatoboa?
Kweli. Hawa watoto huombea hata watumishi wafe ili wapate. Badala ya kutambua wao ndio mizigo katika hili taifa kwa maana hawawezi kuishinikiza serikali yao
 
Mzee Kikwete tayari ana uhalali kikatiba kurudi kugombea urais tena. Mimi ni kati ya watu ambao tunatamani sana arudi.
Kikwete akitaka kurudi nitapiga kampeni nyingi sana hapa jf. Raisi wa maana sana mshua kikwete. Sio hawa tusiowaelewa
 
Kikwete akitaka kurudi nitapiga kampeni nyingi sana hapa jf. Raisi wa maana sana mshua kikwete. Sio hawa tusiowaelewa
Ila kwa kweli huyu wa sasa na waziri wake wa fedha sijui tuwaiteje ili kutunza heshima zao maana nakosa jina zuri.
Haiwezekani wanatapanya hela nyingi kwenye mambo ya zawadi huku watu muhimu hawawajali hata kwa heshima ya uongo.
 
Mtu katumika maisha yake ya ujana kwa taifa, wengine wamepigana hadi vita ndani na nje ya nchi kwa uaminifu mkubwa lakini ndani ya miaka 20 hakumbukwi na hapo kazidi kuwa kikongwe lakini hakuna kiongozi au wabunge (ukiacha Esta Bulaya, Mungu ampe maisha marefu) anaye jali.

Ni tokea Kikwete apandishe pension ya wastaafu wa Hazina toka 25,000 hadi Laki moja miaka 20 iliyopita hajatokea mwingine kuwaza hawa wazee lakini angalia mishahara yao na marupurupu yao leo na miaka 20 iliyopita!

Pengine hata hayo mawazo ya wazee kumuwazia Kikwete arudi madarakani kama Trump yanaweza kuwa sawa, kwanza kiumri Trump ni mzee kuliko Kikwete.

Au mnasemaje kuhusu mawazo haya ya wazee?

Soma makala hii ya Mwananchi utaelewa vizuri
Kiongoz wa Afrika anaongeza malipo / mshahara au Posho kisha anapandisha bei za bidhaa sababu , viongoz hao hao nje ya serikali wana miliki au kuhodhi mihili ya biashara mf biashara ya mafuta ya kuendeshea vyombo hivyo Hata bidhaa zinapanda kisha ulichoongezew hakibadili maisha yako

SOLUTION : Kupambana kuongeza mzunguko wa bidhaa sokoni ili bei iwe stable na affordable na sio hii michezo ya kuficha sukari , mafuta ya kula na mafuta ya kuendeshea vyombo vya moto na mashine za. viwandani .

THE MORE UNAONGEZA MALIPO YA WATUMISHI BILA KUCHEZA UWEPO WA BIDHAA SOKONI BAS NI KUSHUKA KWA THAMAN YA PESA NDO KINACHOFUATIA

MCHELE UKIWA MWINGI SOKON BAS BEI ITAKUWA CHINI

SUKARI IKIWA CHINI SOKON BAS GHARAMA YAKE ITAKUWA CHINI

UNGA UKIWA MWING SOKON BAS BEI ITASHUKA

KUONGEZA MSHAHARA KUMETUTOA KU EXCHANGE 1 KSh kwa 2 Tsh hadi 50 Ksh kwa 500 Tsh

Juz bei zimepanda kenya , serikali yao imeingia Zambia kutafuta maeneo ya kulima kuongeza tani za nafaka sokoni nchini mwao

ila Sisi wamejibu hawana la kufanaya maana duniani kote hali ndo hiyo hiyo sijui Kenya sio Dunian
 
Baba yangu anakula 100,000 kwa mwezi haitoshi inabidi nimuongezee ili amalizie mwezi maskini.
Miaka.30 kapinda mgongo hana hata bima ya afya ..inasikitisha.
 
Hapa nafikiri twende kisayansi kidogo kuliko mihemko na luwatupia lawama za jumla jumla.
Wastaafu wanaozungumziwa hapa ni wale wazee wanaolipwa na Hazina directly na walistaafu miaka ya 90's kwenda nyuma.
Wengi wao wana umri wa miaka 80 na kuendelea au chini ya hapo kama walikuwa kwenye zoezi la redundancy.
Hawa hawajafanya kazi enzi za Kikwete na kuendelea hivyo hawahusiki na mabadiliko yaliyoleta ufisadi, kujilimbikizia mali, maposho ya ajabu na kujipendelea. Wengi labda waingie katika mkumbo wa makosa ya Mwinyi na Nyerere.
Ni aibu kuwatelekeza wazee hao ambao wengine ndio wamepigana vita Uganda, Msumbiji nk au walitumikia kama madaktari,wauguzi,walimu wakati nchi ikiwa na miundo mbinu ya kimasikini kabisa. Yupo daktari mmoja alikuwa ananielezea kuwa katika hospitali moja ya wilaya huko Mtwara kufanya operesheni wakitumia karabai ilikuwa jambo la kawaida, jee leo nani atakubali?
Ni laana kuwatelekeza, usikute ndio maana nchi mambo ni vululu vululu.
Asante. Umeeleza vizuri sana na kuwaelimisha wajinga wanaoandika porojo hapa. Hizo laki wanazolipwa ni lazima zipitie NMB au CRDB ambako kuna makato na tozo
 
Mtu katumika maisha yake ya ujana kwa taifa, wengine wamepigana hadi vita ndani na nje ya nchi kwa uaminifu mkubwa lakini ndani ya miaka 20 hakumbukwi na hapo kazidi kuwa kikongwe lakini hakuna kiongozi au wabunge (ukiacha Esta Bulaya, Mungu ampe maisha marefu) anaye jali.

Ni tokea Kikwete apandishe pension ya wastaafu wa Hazina toka 25,000 hadi Laki moja miaka 20 iliyopita hajatokea mwingine kuwaza hawa wazee lakini angalia mishahara yao na marupurupu yao leo na miaka 20 iliyopita!

Pengine hata hayo mawazo ya wazee kumuwazia Kikwete arudi madarakani kama Trump yanaweza kuwa sawa, kwanza kiumri Trump ni mzee kuliko Kikwete.

Au mnasemaje kuhusu mawazo haya ya wazee?

Soma makala hii ya Mwananchi utaelewa vizuri
Inasikitisha sana. Halafu hao watoa maamuzi na kupanga mustakabali wa Ustawi wa maisha ya Mstaafu wamejisahau kwamba nao pia ni Wastaafu watarajiwa. Hiki wanachokifanya kwa wastaafu wa sasa watakutana nacho wao wenyewe watakapoitwa Wastaafu. Hawana huruma kabisa.
 
Baba yangu anakula 100,000 kwa mwezi haitoshi inabidi nimuongezee ili amalizie mwezi maskini.
Miaka.30 kapinda mgongo hana hata bima ya afya ..inasikitisha.
INASIKITISHA
TENA WAO HAWANA BIMA YA AFYA SAWA NA WENZIWAO
 
Ila kwa kweli huyu wa sasa na waziri wake wa fedha sijui tuwaiteje ili kutunza heshima zao maana nakosa jina zuri.
Haiwezekani wanatapanya hela nyingi kwenye mambo ya zawadi huku watu muhimu hawawajali hata kwa heshima ya uongo.
Kabisa mkuu. Mimi siwaelewi hawa wetu daily matumizi ya anasa kama mandinga makubwa makubwa tu
 
Mama katusikia kilio chetu ametuongeza asilimia 2, kaupiga mwingi tumpe kumi tena.
 
Wastaafu wa serikali wote wana bima ya afya lakini wanaolipwa na Hazina hawana
KWANINI?
 
Hahaha mnaambiwa Deni la taifa limekuwa kubwa hamuelewi, manataka waongeze pension kwa wazee kutoka wapi?

Pension inaongezwa kutoka kwenye makato ya muhusika, kubali ukatwe kiasi kikubwa leo ili upate pension kubwa.

Pension haitokani na kodi au pesa za wahisani, wakitaka nyongeza wakae upya wapitie formular ya kikokotoo. Wapunguze gembe kwa sasa nili waje wafurahi uzeeni.

Hawawezi kupata vyote, huwezi kuwa na elfu kumi ukanywa beer halafu elfu kumi hiyo hiyo ukaitunza. Ni ama uitunze au uinywe beer.

au ongezeni umri wa kustaafu, ili ziwe zina zaa huko mnakotunziwa.
 
Back
Top Bottom