Ni tukio gani la kusikitisha lililowahi kukuta ukiwa night club hadi leo hujasahau

Ni tukio gani la kusikitisha lililowahi kukuta ukiwa night club hadi leo hujasahau

Bata batani

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2011
Posts
3,217
Reaction score
3,694
UKIWA kama mdau wa starehe na mpenzi wa KWENDA night club hebu tujuzane ni tukio gani lililowahi kukuta ndani ya club ambalo hutolisahau.......

Mimi upande wangu ni matukio matatu aisee yaliyowahi kunikuta

1.moja nilisinzia katika makochi nikachomolewa simu na wallet ilikuwa na nauli dah basi nilijikuta mwisho wa Siku natembea HADI Magomeni nikitokea maisha club.

2.tukio LA pili ilikuwaga mambo club KUNA DEMU nilikutana nae nikiwa njee basi nilimlipia kingilio KWA nia ya tuwe wote kama kampani tukiwa ndani lakini mwisho wa siku dem aliniomba ruhusa anaenda chooni basi hakurudi tena nilimpotafuta nilimkuta yupo na njemba nyingine

3.tukio LA tatu KUNA DEMU nilikuwa nakunywa nae bia ila alivyogundua nimeishiwa hela ya bia basi aliamuamua kunikimbia.

Je wewe una tukio gani ambalo uwezi kusahauuu
 
Bidada nilimnunulia kinywaji ili tucheze mziki mpaka basi...nasikitika bando la vinywaji lilikata na njiwa akapeperuka halafu nilikuwa na hamu nae sana
Halichachi
 
Kuna dem mmoja aliniomba nimpeleke club yeye na rafiki yake kwa kuwa tangu waje hapa Dar hawajawahi kwenda... Basi huyoo nikaweka wese kwenye kigari changu mpaka Maisha. Kufika kule mtoto akawa hataki kucheza na mi huku rafiki yake sina mzuka naye. Hasira zilizonishika nilitaka niwatelekeze pale club warudi kwao Makongo juu kwa mguu... Baadaye huruma ikaniingia ikabidi tu niwe mpole. Mpaka nawarudisha mida ya saa nane usiku, nilikuwa nahesabu hasara kama ya elfu sitini niliyounguza toka kwenye mshahara wangu wa laki nne na nusu... that was way back in 2010!
 
Ha ha ha ha ha. Nikiwa club Hapo Next door siku aMbayo walikuwa wana perform Navy Kenzo,aisee ukumbi ulijaa sanaa full kukanyagana na kusukumana then ukumni ulivyojaa mpaka AC zikawa zime zidiwa like zilizimwa kumbe ziko ON,nili sweat Sana nikanunua chupa 4 za maji ya kunywa yet I felt nothing done kwenye koo,joto lilikuwa Kali plus hewa nzito nilihisi nataka kuzimia. Nikatoka nje,nilsikitika Sana ile siku,Maana Hata show wenyewe siku imalizia in short siku enjoy,nili boreka
 
Mara zote klabu nilikua naenda kama mlinzi.
Siku hiyo kuna mdada analeta ukorofi pale MK, mwenzangu akamsomba begani anamtoa nje nyuma anafuata brazamen akimsihi jamaa amshushe mpenzi wake, nikafuatia mimi nyuma.

Kufika nje mlinzi mwenzangu akamrusha mdada, mimi nikahamaki kwakua hiyo siyo namna ya kumhandle mteja. Bwana wa mdada akawa ananiambia kwa kelele "Mwambie mwenzako nitampasua mi siogopi mwili"
Yule mwenzangu akajibu "We fala tu toka hapa ms.nge wewe"

Yule brazamen akachomoa bunduki, pale pale akili ikawa inanishawishi nichomoke lakini miguu haina nguvu, mwenzangu alivyoona bunduki akapiga magoti anaomba msamaha.

Yule brazamen akatoa maneno ya shombo, akatamba weee, alivyomaliza akamchukua demu wake wakaingia ndani ya gari kibati.
 
Wakati nasoma , Siku hiyo tumekusanyana kikundi chetu kama wa 4 ivi tunaenda Maisha..kiukweli mimi sikuwa mzoefu na tungi a.k.a ulabu ila wenzangu walikua ni wazoefu sana tuu maaana walikua wanakunywa ndo waningia class..Sasa tumeingia na mimi kujifananay oya oya tukaanza kuzishusha bhana..vitu kupanda kichwani nikaanza kujiona mbabe kila demu nataka nimbambie nikakutana na demu flan hiv anacheza pekeyake tuu kumsogelea sogelea ile kumletea kisura cha mapenzi kumbe pembeni alikua baunsa mmoja ndo bwana aake ..jamaa akanifata kiustaarabu tu kunitoa nikajifanya namletea mbovu ..yule jamaa alinipa Box moja nikaenda kuangukia pembeni na makochi nimechanika tayari shingoni nikamtapikia mdada mmoja ivi kwenye kochi hapo sijui washkaji wakwapi Yule dada nilihisi ni malaika ..akaninyanyua hadi akanipeleka washroom akanisafisah fresh yan akanunua maji halaf akani toa hadi nje kupata upepo nikawa nimemlalia mapajani ..Hadi kunakaribia kukucha akachukua bajaji hadi gheto kwake kumbe alikua ni mwanafunzi wa IFM....itaendelea
 
Mkuu nitakutafuta... Na Mimi nataka niwe baunsa
 
Nasubir
 
Nakumbuka nipo miaka 18 nilichukuwa gari(Land Cruiser) ya mzee na washkaji zangu 3 wote tukiwa 4. Hapo ndio kwanza naanza kunywa pombe sasa nilikuwa nakunywa bia ila siku hii nikasema wacha ninywe Konyagi, Dadeki Nilimuona mdada akicheza nikamzukia na kucheza nae. Baada ya dakika 30 nikambeba mpaka nje kwenye gari nikamla uroda, sasa nilikuwa nasikia harufu ya samaki mwilini mwa huyu dada lakini nilikuwa nipo katikati ya mchezo. Kumaliza tukarudi ndani club nawaona rafiki zangu wamekaa na kaka yake demu wangu huku wakinicheka. Ndio wakanipa story kuwa yule mdada alikuwa mamantilie(muuza samaki), Uzuri wa kaka wa demu wangu hajamwambia nilichokifanya mdogo wake. Ila alini tahadahrisha kunywa pombe kupita kiasi na kuniambia kama kuna maradhi na hataki kumuona mdogo wake akiambukizwa. Siku hio ilikuwa ndio mwisho kunywa konyagi nilibaki na bia tu nazo pia nimeshawacha.
 
Aina haja ya kusubiri mkuu nenda kalale ni mimi huyo mdada
Ni hivi tulikuwa tunasoma chuo kimoja so nikamsaidia kama mwanafunzi mwenzangu nikamkodishia bajaj nikamrudisha hostel kwao nami nikaenda zangu kulala kesho akanishukulu kwa msaada niliompa ni hivyo tu hakuna jingne
Haya nenda kalale nakuona unasinzia hapo
 
Dah kumbe una roho ya ukarimu hvyo
Kwahyi siku hiz umeacha kwenda club ili nijiangushe hata kwa bahat mbaya
 
Miye naumia tu hasa nikiona vijana wenzangu ambao tulikuwa nao na tulianza nao ujana pamoja Leo hii unawakuta wamechoka wakati enzi zile mnakula bure mnalala bure kipindi mnasoma shule ya msingi darasa la saba saba hivi ndio mnakuwa kuwa sasa hapo nadhani mnajua kwakuwa wadogo nyumbani wanabana basi wenzenu club tulianzia disco toto

Kila juma pili lazima upitie jamaa zako hao disco toto kuanzia saa kumi jioni hiyo acha tu enzi bolingo inatamba enzi small jobiso anatusumbua watoto wenzake, Maana kila mtoto alitaka acheze kama small jobiso ingawa small tulimzidi umri kidogo

Yani nakumbuka matukio kati kati ya burudani dj anazima mziki inatagaza show mtoto atakaye shinda basi atapewa zawadi mnakumbuka ghato ule wimbo azalaki The hawa ebwana basi siunajua zile style ilikuwa ndio balaa, au kanda bongo man kitu in the morning hatari , ikifika mda Wa kuvunja sasa sikuhizi mnasema kushake ebwana zikipigwa ngoma za wako jako michael jackson balaa hapo uniambii kitu yale mafank kamon kamon aooo ooooh aoooh du hapo nimekumbuka disco toto yani wewe kama umepita uku alafu bado ujaoa au kuolewa unaitaji maombi

Nakumbuka ilikuwa ikifika saa kumi Na mbili jioni disco toto mwisho nyumbani ukifika nyumbani sasa unaanza kucheza style ulizoiga club haa haa hatarii

Haya sasa tuje club za ukubwani upo sekondari hapo, chuo sasa uwi yelewii hakuna nachokumbuka zaidi ya kupoteza PESA zangu tu maana foolish age ndio imekolea mda huu

Yani sasa inabidi tuachie vijana haya mambo maana ukitizama hakuna tulichopata tangu utoto mpaka leo hii starehe haijanipa faida yoyote

Maana nakumbuka loyal pamoz mbeya, delux mwanza, copa cabana Mwanza, Triple A arusha, mungano mess, mwanaisungu, Tabora, bills dar hizo sehemu sujui kama bado zipo Leo hii

Maana leo arusha kuna club D,, mwanza kuna rock bottom, fussion juzi kati nimeenda mwanza hiyo fussion nikaona jina jipya, haya mbeya nilienda nikakuta maisha club yani kumekuwa Na club kibao ukienda dodoma sasa napo balaa Haya ukija dar ndio balaa club kila kona sasa jamani tola mda huo mpaka leo si pumzike tu

Tukio nalokumbuka siku moja nimerudi likizo kutoka shule nipo nyumbani akatokea msichana ambaye nilisoma naye shule ya msingi kapendeza basi tukapiga story nini akaomba jioni tutoke twende mziki maana mziki ilikuwa sehemu Ya maisha yetu tangu udogo kweli ile jioni hao club kufika kule nikakutana Na jamaa yangu tu wa mtaani akamtolea macho yule class mate wangu nikamwambia kama anamuitaji asimamie show ya vinywaji dem akilewa pouwa basi bwana jamaa akasimamia show ilipofika mida ya kuondoka nikamwambia jamaa ongea name sasa jifanye miye sijui kitu kinachoendelea kweli wakaongea wakayajenga so wakapotea ikawa kama wamenikimbia kwakua nilikuwa najua nikarudi nyumbani peke yangu kesho yake asubuhi nilikuwa narudi shule basi nikarudi shule, kipindi cha likizo narudi tena nakuta jamaa na yule dada wanaishi wote kama mme na mume yani navyo andika hivi sasa wana watoto wawili

Kiukweli matukio yote hayo nawaza pesa nilizopoteza nashukuru sasa nimeokoka naenda club ya yesu.
 
Back
Top Bottom