Ni tukio gani la udogoni ambalo huwezi kulisahau?

Ni tukio gani la udogoni ambalo huwezi kulisahau?

Choo cha shimo! Nikiwa mdogo like 6 yrs nikaletewa nguo mpya shati na kaptura yake nikaivaa siku hiyo hiyo, baada ya muda nikabanwa na haja kubwa nikaenda msalani nikafanya yangu baada ya kumaliza nikawa naiangalia kaptura yangu mpya!!! Hamadi ikaniponyoka ikadumbukia chooni haaa nihaha nikatafuta mti n utoto wangu najaribu kuitoa kumbe ndo nazidi kuisokomeza nikabaki nalia tu

Kwenda kwa babu kutoa taarifa wee nilichezea bakora sitasahau. Ajabu kile choo baada ya muda kikabomoka eti nikaenda kuitafuta kwenye yale mabaki[emoji851][emoji851]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee utoto bwana hatar , kuna mjamaa alikua ni mlinzi ws disco enzi hizo basi sisi wazee wa vitongo tukawa tunataka tuingie kws njia za panya si akatunasa bas akampa kipigo mwenzangu daah mm nikachomoka aisee

Sku tunarudi game flani hivi ya mpira tukamkuta njiani kaomgozana na mke wangu

Tulimpa kipigo cha mbwa koko hadi mkewe akataka kuzimia kwa mayowe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sinto sahau nilipo shuhudia mke wangu akijifungua huku aki"push", na usiku wake nikapata ndoto nasikia maneno yale "pushhh" yakijirudia.......
Asubuhi nilipo amka, nikakuta kweli nime"pushh" haja kubwa kwenye bed yote....[emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12]
[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka hio niko around 4yrs. Nyumbani tulikua tunawangiwa vibayaa sana mama alikua anawasikia wanatoka juu ya dari wanadondokea barazani akiwasha kibatari anaona mkono unazima taa.
Siku moja wachawi waliniiba usiku wakaniweka chini ya mtungi mama akaniona asubuhi. Sijui walinifanya nini usiku huo mpaka leo
 
Nakumbuka nikiwa darasa la nne nilimtongoza binti ananizidi umri yupo darasa la 7 enzi hizo tunaita LY, kumbe hakupenda akaleta ushahidi wa barua kwa mama, Mama akatoa amri nilale chini nichapwe na huyo binti niliyemtongoza na akamwambia akilegeza mikono kunichapa kizembe atamchapa na yeye, kidume nikala fimbo zakutosha.
Yule binti ninamchukia hadi leo sijui yupo hai huko alipo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tulienda shambani sasa mchana nikapiga ulanzi wa kutosha kumbe ulanzi na jua ni vitu viwili tofauti... ile narudi jua kali joint za miguu zikaanza kua loose yaan natembea napepesuka kama feni la muhindi lililoharibika bearing.... aisee sitasahau kamwe
 
Back
Top Bottom