Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Kuna siku mimi na marafiki zangu tuliendaga shamba la shule tukaiba tikiti. Tulichagua kubwa kuliko yote, tulikuwa watu wannne na lile tikiti lilikuwa kubwa ikabidi tukatafute wheelbarrow tuje kulibeba. Basi bwana sisi hao na wheelbarrow letu, sasa tukiwa tunaelekea dorm kuna mlinzi alituona akaanza kutukimbiza tukakimbia na tikiti letu hadi room. Lakini kumbe yule mlinzi aliniona na shule kipindi hiko najulikana shule nzima.
Sasa bwana tumefika na lile tikiti chumbani tukalificha kwanza chini ya kitanda kwamba tukitoka dinner tuje kulikata. Sasa ghafla mwalimu wa zamu bwenini akaja kuniita akaniambia nimtajie wenznagu tuliokuwa shambani na kuna kitu tuliiba ikabidi niwataje wana. Sasa tuko dining tukatajwa majina tukasimamishwa alafu shule yule ilikuwa ni mixed gender. Kwanza hapo tuko form 3 tumedhalilishwa mbele ya vinjuka, tukapewa na adhabu. Basi baada ya kumaliza adhabu yetu tkarudi room tule tikiti tumefika kulipasua lile tikiti ni bichi ndani aise machozi yalinilengalenga nilitamani kupiga ukunga.